Kufungwa kwa kiwanda

on .

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE

/* Style Definitions */ table.MsoNormalTable {mso-style-name:"Table Normal"; mso-tstyle-rowband-size:0; mso-tstyle-colband-size:0; mso-style-noshow:yes; mso-style-priority:99; mso-style-qformat:yes; mso-style-parent:""; mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt; mso-para-margin-top:0in; mso-para-margin-right:0in; mso-para-margin-bottom:10.0pt; mso-para-margin-left:0in; line-height:115%; mso-pagination:widow-orphan; font-size:11.0pt; font-family:"Calibri","sans-serif"; mso-ascii-font-family:Calibri; mso-ascii-theme-font:minor-latin; mso-fareast-font-family:"Times New Roman"; mso-fareast-theme-font:minor-fareast; mso-hansi-font-family:Calibri; mso-hansi-theme-font:minor-latin;}

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AKIFUNGIA KIWANDA CHA SARUJI

Na Alice Mapunda,Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda  amekifungia kiwanda cha Saruji kinachofahamika kwa jina la Arusha Zaidi Cement Company  kilichopo eneo la Ngaramtoni jijini Arusha   kutokana na uendeshaji wa kiwanda hicho kugubikwa na utata kuanzia kwenye uzalishaji,wamiliki na mazingira kutokuwa na usalama kwa wafanyakazi wake.

Mkuu huyo wa Mkoa amefanya ziara ya kushtukiza akiambatana na maafisa wa Mamlaka ya Ukusanyaji wa Mapato TRA ndipo alipobaini kuwa kiwanda hicho kimekua kikikwepa kulipa kodi hivyo kukifunga kwa muda usiojulikana.

Kufungwa kwa kiwanda hicho kumesababishwa na ukiukwaji wa taratibu za uwendeshaji wa viwanda ikiwemo kuwapatia maziwa wafanyakazi wote ilikuwakinga na magonjwa mbalimbali yakiwemo kifua kikuu.

 Aidha amemtaka mmiliki wa kiwanda hicho ambaye hakufahamika mara moja kuhakikisha kuwa anafika kwenye Ofisi za mkuu wa mkoa kutoa taarifa ya kiwanda hicho pia ameuagiza uongozi wa mkoa kwa kushirikiana na Wataalamu wa mazingira kufanya tathmini ya mazingira kwani kiwanda hicho kinachangia uharibifu wa mazingira.

‘Ukiuliza mmiliki wa kiwanda hiki ni kigugumizi haeleweki,mazingira haya si salama na uendeshwaji wa shughuli za hapa bado una utata hivyo naagiza kiwanda hiki kifungwe mara moja kuanzia hivi sasa na wafanyakazi wote waende majumbani” Alisema Ntibenda.

 Moja kati ya Viongozi wa kiwanda hicho ambaye hakufahamika jina lake mara moja amekanusha na kudai kuwa wamekua wakilipa kodi kwa serikali huku akikataa kuzungumza na waandishi juu ya wamiliki wa kiwanda hicho.

Serikali imekuwa ikipoteza kodi nyingi kutokana na viwanda bubu vinavyokwepa kodi,juhudi zakuhakikisha viwanda hivi vinatambulika na hatua kali zinachukuliwa dhidi yao ikiwemo kuvifungua au kulipa kadi na faini.

Bonus William Hill
Bonus Ladbrokes
Premium Templates