Katibu Tawala wa Mkoa, Richard Kwitega amekabidhi zawadi za Eid Al Fitr kwa mahabusu ya watoto kwa niaba ya Muheshiwa rais wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania.
Amesema, muheshimiwa rais ametoa zawadi ya Mbuzi dume,Mchele kilo 25 na mafuta yakupikia lita 10.Vitu hivyo vitawasaidia watoto hao katika kusherekea sikukuu hiyo.
Aidha amewapa salamu za rais kwa kuwataka wajuwe mahali pale nipa mda mfupi tu hivyo wakitoka wanatakiwa wakawe raia wema na wakujituma zaidi katika kazi na wale ambao ni wanafunzi wakakazane zaidi na shule.
Wakitoa shukrani zao, watoto hao wamemshukuru sana katibu tawala kwa niaba ya rais, na wamempongoze kwa kazi nzuri anayofanya katika kujenga taifa hili na wao wameaidi wakitoka hapo watakuwa raia wema.
Pia watoto hao wameiyomba serikali kuwasaidia katika usikilizwaji wa kesi zao zisichukue mda mrefu sana na hivyo kupelekea wengi wao kukosa masomo yao ya shule.
Mkurugenzi wa kituo hicho Musa Mapua, amesema tokea mwaka huu uwanze jumla ya watoto 48 wameshapita katika kituo hicho na kwasasa wapo 11 tu na wote niwakiume.
Amesema Changamoto kubwa wanayokabiliana nayo kituoni hapo ni ukosefu wa gari lakubeba watoto hao palewanapoitajika kupelekwa mahakamani na ukosefu wa uzio kwa usalama wa watoto hao.
Hivyo ameiyomba serikali kukisaidia kituo hicho ili watoto hao wawe katika hali ya usalama zaidi.
Kila mwaka muheshimiwa rais amekuwa akitoa zawadi mbalimbali za eid katika maeneo mengi ya nchi kwa lengo lakushiriki na walengwa katika kusherekea sikukuu hiyo.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa