WAZIRI MKUU AKIWA ZIARANI NGORONGORO

on .

Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa NCCA na balaza la wafugaji wilayani Ngorongoro.

Watumishi wa Mmalaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) wamepigwa marufuku kuingiza mifugo yao katika hifadhi ya bonde la kreta.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofanya kikao na watumishi wa Mmalaka pamoja na balaza la wafugaji wa Ngorongoro.

Utalii umeshuka sana nchini na hii imesababishwa na ongezeko la watu na wanyama katika hifadhi  ya bonde la kreta na hivyo kupelekea watalii wengi kushindwa kuona wanyama badala yake wanaona ng’ombe na watu hii inawakatisha tamaa kwakuwa wao wanapenda kuona vivutio vyetu ambavyo ni wanayama pori.

Watumishi wenyewe wa mamlaka  ndio wanaongoza kwa kuingiza mifuko ambao wanawatumia watoto wadogo washuke bondeni kreta na ng’ombe hao kwa lengo lakujipatia maji na udongo wa chumvi chumvi.

“Kwanzia leo ni marufuku kwa mtumisho yoyote kupeleka mifugo yake kwenye malisho kule bondeni na hata pia kwa wageni wengine”,alisema.

Mifugo ya wenyeji wa Ngorongoro inayoingia bondeni ni kidogo ukilinganisha na ile ya wageni kutoka maeneo mangine ya jirani na hifadhi.

Amewashauri balaza la wafugaji kushirikiana na serikali kwakufanya sensa ya watu na wanyama katika hifadhi iliisaidie kutambua wenyeji na wageni na kwa mifugo iwekewe alama .

Akifafanua zaidi Waziri wa maliasili na utalii Jumanne Magembe alisema tayari wizara imeshamtuma mtaalamu ambae anatafuta maeneo yenye maji yanayoweza kupatikana kwa wingi katika maeneo ya  nje ya hifadhi ili kupunguza wanyama wanaoshuka katika bonde kwa lengo lakupata maji.

Mkurugenzi wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Fredi Manongi alisema kuna upungufu watalii waliongia katika kreta kutoka 592494 kwa mwaka 2014 hadi kufikia 589374 kwa mwaka 2015  na sababu kubwa ni ongezeko la mifugo na watu katika kreta na kuna magugu mengi ndani ya kreta.

Pia kulikuwa na ubadhilifu sana kwenye mfumo wa malipo hasa kwa wageni waliokuwa wanataka kuingia hifadhini na ambayo imesababisha kushuka pia kwa mapatoka katika hifadhi.

Aidha Majaliwa amewapongeza balaza la wafugaji kwakutambua umuhimu wa hifadhi hiyo kwakuweka wazi changamoto mbalimbali zilizopo nakusisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao katika kukuza hifadhi hiyo na kumtaka mkurugenzi wa hifadhi bwana Manongi kuendelea kurudisha nidhani kwa watumishi wa hidhafa hiyo.

Ambayo itasaidia kuongeza mapato kwa serikali na hata idadi ya watalii itaongezeka nchini kwa nidhani ya watumishi ikirudi kama inavyotakiwa hasa kwakuongeza bidii kwenye utendaji wao wa kazi.


Baadhi ya watumishi wa NCCA na balaza la wafugaji wakimsikiliza Kassim Majaliwa katika ukumbi wa NCCA,Ngorongoro.

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Arusha wakimsikiliza Waziri Mkuu Majaliwa(hayupo pichani) alipokuwa akifanya kikao cha majumuisho baada ya ziara yake katika Halmashauri tatu za Mkoa wa Arusha.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo baada yakufanya ziara yake katika halmashauri tatu za Mkoa wa Arusha.

Bonus William Hill
Bonus Ladbrokes
Premium Templates