WAZIRI MKUU,KASSIM MAJALIWA AFANYA KIKAO NA WAFANYABIASHARA WA JIJI LA ARUSHA.

on .

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyabaishara wa Jiji la Arusha katika ukumbi wa AICC,Arusha.

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE

/* Style Definitions */ table.MsoNormalTable {mso-style-name:"Table Normal"; mso-tstyle-rowband-size:0; mso-tstyle-colband-size:0; mso-style-noshow:yes; mso-style-priority:99; mso-style-qformat:yes; mso-style-parent:""; mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt; mso-para-margin-top:0in; mso-para-margin-right:0in; mso-para-margin-bottom:10.0pt; mso-para-margin-left:0in; line-height:115%; mso-pagination:widow-orphan; font-size:11.0pt; font-family:"Calibri","sans-serif"; mso-ascii-font-family:Calibri; mso-ascii-theme-font:minor-latin; mso-fareast-font-family:"Times New Roman"; mso-fareast-theme-font:minor-fareast; mso-hansi-font-family:Calibri; mso-hansi-theme-font:minor-latin;}

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Mjaliwa amewata wafanyabiashara kuwekeza zaidi kwenye sekta mbalimbali hasa za viwanda hapa nchini.

Aliyasema hayo alipokutana na wafanyabiashara wa jiji la Arusha nakuwashauri wawekeze kwenye mikoa yote ya Tanzania hasa kwakuanzisha viwanda,ilikujenga nchi ya viwanda kama dhamira ya serikali ilivyo.

“Nawashuri muwekeze kwenye mikoa yote hapa nchini na niruksa kabisa viwanda vingi vianzishwe”.

Hata hivyo amewata waendelee  kushirikiana na serikali yao ya awamu ya tano kwakuwa ipo pamoja nao na inaongeza ulinzi zaidi kwa wafanyakazi wote nchini ili wawe na amani na waweze kuwekeza zaidi.

Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuboresha zaidi kwenye sekta binafsi hasa kwakupambana na wasiolipa kodi ili walipe nakuweka usawa katika biashara na kukuza ushindaji wa biashara.

Aidha Majaliwa amewataka watendaji wa serikali kuvilinda viwanda vya ndani kwakuhamasisha matumizi  ya rasilimali za ndani napia kuzipunguzia ushuru ili viwanda viweze kukuwa kwa kasi kama serikali inavyodhamiria kujenga nchi ya viwanda.

Majaliwa bado anaendelea na ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Arusha kwa kutembelea halmashauri zote za Mkoa.

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo(Kulia) na mwenyekiti wa CCM Mkoa Lekule Laiza(kushoto)katika mkutano na wafanyabiashara wa jiji la Arusha,AICC Arusha.

 

SAMIA SULUHU ATEMBELEA KIWANDA CHA MT. MERU MILLERS

on .

Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo ya malighafi inayotumika katika kutengenezea mafuta yatokanayo na alizeti katika kiwanda cha Mt. Meru Millers, jijini Arusha.

Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassani ametembelea kiwanda cha Mt. Meru Millers Limited  cha jijini Arusha kinachojishughulisha na utengenezaji wa mafuta yatokanayo na alizeti.

Akizungumza baada yakujionea uzalishaji wakiwanda hicho,amesema lengo kubwa ya ziara yake katika kiwanda hicho ilikuwa nikujionea shughuli zinazofanywa na kiwanda hicho.

Pia ameweza kusikiliza changamoto mbalimbali zinazozikabili kiwanda hicho na kubwa ikiwa ni utozwaji wa kadi nyingi na serikali itahakikisha kunakuwa na utaratibu mzuri wa ulipaji wa kodi hizo.

Aidha alisisitiza zaidi kuwa serikali ya awamu wa tano imedhamilia ujenzi wa viwanda vingi nchini ambavyo vitatumia malighafi za ndani ya nchi nakukuza uzalisha kwa wakulima na hata pia kutoa ajira za kutosha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mt. Meru Millers Atul Mittal alisema ikiwa serikali itapunguza kodi hizi nyingi itasaidia ukuwaji wa viwanda vilivyopo na hata kuhamasisha wawekezaji wengine kuwekeza kwenye viwanda hapa nchini.

Makamu wa Rais yupo Mkoa Arusha kikazi kwa mda wa siku 3 ambapo atendelea kutembelea viwanda vya mkoani  hapa na pia atazindua jengo la Mahakama ya Afrika.

 

ZIARA YA RC GAMBO MAKUYUNI

on .

 
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo akihutubia wananchi wa kijiji cha Esilalei katika tarafa ya Makuyuni Wilayani Monduli.
 
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameiagiza halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kupitia upya taratibu na kanuni zilitumika kwenye umiliki wa shamba la Manyara Ranch lililopo tarafa ya Makuyuni.
 
Alisema hayo alipofanya ziara ya siku moja katika tarafa hiyo nakutembelea shamba la Manyara Ranch ambalo wananchi wanadi ni mali yao baada ya umiliki wake kufutwa mwaka 1999 nakurudishwa kwa wananchi.
 
Hata hivyo bado kuligubikwa na maswali mengi ya hati miliki ya shamba kuandikwa jina la Tanzania Land Conversation Trust (TLCT)  ambacho ni chombo cha kusimamia shamba hilo na badala ya mmiliki mkuu ambae ni Halmshauri ya Wilaya ya Monduli, hali iliyopelekea Gambo kutolea maamuzi ya hati miliki iandikwe Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
 
“Naiagiza Halmashauri kuhakikisha hati miliki ya shamba hili isomeke jina la Halmashauri badala ya TLCT kwasababu tayari shamba lilisharudishwa kwa wananchi na halmashauri ndio msimamizi wa mali za wananchi”,alisema.
 
Akisoma taarifa fupi ya shamba la Manyara Ranch Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya African Wildlife Foundatio(AWF)ambao ndio wanaendesha shughuli zote katika shamba hilo bwana Fidelisi Ole Kashe amesema taasisi hiyo iliingia mkataba wakuendesha shughuli zote ndani ya shamba kutoka kwa TLCT baada ya chombo hicho kushindwa kuziendesha.
 
Aidha akifafanua zaidi Mkurugenzi mtendaji wa TLCT bwana Boniface Ngimojiro alisema TLCT iliundwa na bodi ya halmashauri ya wilaya ya Monduli ili isimamie na kuendesha shughuli zote za shamba la Manyara Ranch na baada yakushindwa kuendesha ndipo wakazikabidhi kwa AWF.
 
Hata hivyo Gambo alisema ataunda timu yakuchunguza shughuli zote za TLCT kwa mda wa miaka 10 ya nyuma ilikusaidia kufahamu zaidi kama chombo hicho bado kinahitajika katika uwendeshaji na usimamizi wa shughuli za shamba la Manyara Ranch.
 
Gambo amekuwa akifanya ziara zake katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha kwa lengo lakusikiliza kero mbalimbali za wananchi zinazowakabili.
 

Mkurugenzi Mtendaji wa AWF akisoma taarifa fupi ya mradi wa shamba la Manyara Ranch kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(hayupo pichani),pembeni yake (kulia) ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard Kwitega akifuatilia taarifa hiyo.
 
Wananchi wa kijiji cha Esilalei wakiwa kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akijibu hoja mbalimbali za wananchi wa Makuyuni alipofanya ziara katika tarafa hiyo iliyopo Wilayani Monduli.
 

GAMBO APOKEA MIFUKO 200 YA SIMENTI KUTOKA KWA WAMILIKI WA MAGARI YA NOAH ARUSHA

on .

 

 

 

Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo akipokea mifuko 200 ya simenti kutoka kwa chama cha wa wamiliki wa magari aina ya Noah cha Jijini Arusha.

 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akimkabidhi mifuko 50 ya simenti Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo kwaajili ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Oldeani Wilayani Karatu.

 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akimkabidhi mifuko 50 ya simenti Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo kwaajili ya ujenzi wa kitua cha afya Namanga, Wilayani Longido.

GAMBO ASHIRIKI UJENZI WA DARAJA FUPI

on .

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE

/* Style Definitions */ table.MsoNormalTable {mso-style-name:"Table Normal"; mso-tstyle-rowband-size:0; mso-tstyle-colband-size:0; mso-style-noshow:yes; mso-style-priority:99; mso-style-qformat:yes; mso-style-parent:""; mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt; mso-para-margin-top:0in; mso-para-margin-right:0in; mso-para-margin-bottom:10.0pt; mso-para-margin-left:0in; line-height:115%; mso-pagination:widow-orphan; font-size:11.0pt; font-family:"Calibri","sans-serif"; mso-ascii-font-family:Calibri; mso-ascii-theme-font:minor-latin; mso-fareast-font-family:"Times New Roman"; mso-fareast-theme-font:minor-fareast; mso-hansi-font-family:Calibri; mso-hansi-theme-font:minor-latin;}

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo ameshiriki ujenzi wa daraja fupi(drift) katika kijiji cha Orgirah kata ya Mundarara na tarafa ya Engarenaibow kwa lengo lakuhamasisha wananchi na viongozi wengine.

Akitoa msisitizo kwa viongozi kujitoa sana pale wanapoitajika kushiriki shughuli mbalimbali za  maendeleo kwa wananchi wao hasa zile ambazo zimeanzishwa kwa nguvu za wananchi wenyewe.

“Viongozi mbalimbali wasiwe wazito kujitoa katika shughuli kama hizi za maendeleo ya wananchi na hasa ambazo zimeanzishwa kwa nguvu za wananchi wenyewe nivema basi na serikali nayo kupitia viongozi kwa ngazi tofauti kujitokeza nakuunga mkono”.

Mradi huo wa daraja fupi(drift) ulianza rasmi mnamo Octoba ,2016 kwa lengo lakuunganisha vijiji viwili vya Orgirah na Igulailungwa ambavyo vilitenganishwa kwa ukosefu wa daraja hilo fupi na kupelekea kwa vijiji hivyo kukosa mawasiliano.

Aidha mradi huo mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha shilingi milioni 9 ambapo mpaka sasa ni milioni 6 tu ndio zimetumika katika ujenzi huo, ikiwa Halmashauri ya Wilaya ya Longido ilichangia 450,000, Mkurugenzi wa halmashauri alichangia 640,000 na nguvu za wananchi ni milioni 5.

Hata hivyo Gambo aliwapongeza wananchi hao kwa juhudi walizozianza za ujenzi huo na hivyo serikali itawasaidia pale penye mapungufu na wananchi wenyewe wanatakiwa kujitokeza zaidi hususani kwenye shughuli kama hizo za maendeleo.

Mradi huo bado unamapungufu ya shilingi milioni 2 ili kukamilisha milioni 9 kama gharama nzima ya ujenzi na Mkuu wa Mkoa aliaidi kuchangia mifuko 30 ya simenti,pesa taslimu 500,00 na kutoa katapila ikiwa wananchi watakuwa tayari kuchangia mafuta. Meneja wa TANROAD Arusha Enginia John Kalupale aliaidi kuchangia mifuko 50 ya simenti.

Pia mwenyekiti wa chama cha CCM Mkoa Lekule Ole Laiza atachangia mifuko 30 ya simenti, mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido bwana Sabore Molleimet atachangia 500, 000, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido  Juma Muhina nae atachangia 400,000 na Halmashauri yenyewe itaenda kujadili kwenye vikao vyake namna yakusaidia ujenzi huo.

Gambo bado yupo ziarani Longido huku akishirikiana na wananchi wa Wilaya hio katika shughuli mbalimbali za maendeleo yao.

HHHili ndilo daraja fupi(drift) lililojengwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji cha Orgirah.

Bonus William Hill
Bonus Ladbrokes
Premium Templates