Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha zimehamasishwa kutenga maeneo maalumu kwaajili ya ujenzi wa viwanda kama maelekezo ya serikali ya awamu ya tano yanavyoelekeza.
Ameyasema hayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo alipokuwa akizungumza na viongozi wa halmashauri zote za mkoa wa Arusha kwa lengo lakuweka mikakati yakiuntendaji hasa kwa mwaka wa fedha unaokuja 2017/2018.
“Nazitaka halmashauri zote zieleze hapa namna zilivyojipanga kwa mwaka wa fedha ujao katika kutekeleza adhima ya serikali ya viwanda,bainisheni maeneo mliyotenga na muelezee hali ya miundo mbinu ya msingi ilivyo,lina ukubwa gani,lina hati au halina hati na niaina gani ya kiwanda mmependekeza.”
Aidha amewata watumishi wote wa serikali kubadilika kwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake kila mtu afanye kazi kwa bidii hasa kwakutekeza malengo ya serikali.
Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote ambae atakwamisha malengo ya serikali hivyo hatua zakitumishi zitatumika kwa mtumishi huyo ili kukuza ufanisi sehemu za kazi.
Gambo anaendesha kikao cha siku 3 kwa kupitia mipango mbalimbali yakila halmashauri nakushauri nini kifanyike kwa mwaka wa fedha ujao.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa