TASAF:
Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikao ambayo imeratibu mradi wa kunusuru kaya maskini kwa awamu ya 1 na ya 2.Mradi huu ulianza rasmi Julai 15, 2014, nakuhususha wadau mbalimbali kwa lengo la kutoa uwelewa zaidi kwa wadau wa mradi huu.
Lengo la mradi huu nikuziwezesha jamii kubuni miradi midogo ambayo itawasaidia kuwainua kutoka mazingira ya umaskini.Kaya ambazo zilipewa kipaombele ni zile zenye makazi duni,watu binafsi wenye wanaoishi kwenye mazingira magumu na kaya zilizokosa chakula.
Jumla ya Kaya 503 zimenufaika na miradi midogo midogo ambapo kaya 225 zimenufaika na miradi ya TEHEMA na kaya 450 zimenufaika na miradi midogo ya VG na jumla ya shilingi 5,927,610,027.91 zilitumika katika miradi hiyo.
Pia Mkoa wa Arusha umekuwa miongoni mwa mikoa miwili ambayo imeendesha mradi mwingine wa OPEC III,mkoa mwingine ukiwa ni Njombe kama mikoa ya mifano. Jumla ya miradi midogo midogo 63 imeshakamilika katika mkoa wa Arusha na kwa wilaya za Arusha, Karatu,Monduli,Longido, Arusha Jiji, Meru na Ngorongoro ambapo kila wilaya imepata miradi 9 chini ya mpango huu wa OPEC III.
Mradi huu imefadhiliwa na umoja wa nchi zinazosafirisha mafuta,na umeweza kufikia katika halmashauri 13 kwa mikao miwili ya Arusha na Njombe kwa lengo lakufikia vijiji/Mitaa 600.
Mpango mkubwa zaidi wa mradi huu nikuwawezesha wananchi waweze kupata fursa mbalimbali za zakiuchumi na maisha.Ambapo kwa jamii zilizokosa kabisa huduma zakijamii kama vile; elimu,maji afya na ukosefu wa ajira,mradu huu uliweza kutoa fursa za ajira za mda.
Kwa Mkoa wa Arusha mradi huu umeweza kutoa fursa katika maeneo ya miundo mbinu,nafasi za kazi za umma na vikundi vyakukopeshana.
Kuanzia Julai/Agosti 2015 hadi Machi/Aprili 2017 jumla ya kaya maskini 62,492 zilibainishwa kutoka kwa wilaya zote 7 na kaya 46,771 ikiwa (wanaume 5,059 na wanawake 41,712) walibainishwa, na TMU walitoa kiasi cha fedha cha shilingi 22,370,584,090.91 kwa malipo ya vijiji/mitaa 290.Ikiwa miradi midogo midogo ya miundombinu iliyokwishaanzishwa 14 ipo kwenye hatua mbalimbali zakukamilika.
OPEC III umeweza kutoa fursa ya miradi midogomidogo 63 kuanzishwa na kila Wilaya ndani ya Mkoa wa Arusha umeweza kupata miradi 9 ambayo ipo katika hatua mbalimbali zauwendelezwaji na zimegharimu kiasi cha shilingi 2,748,468,978.39.
Aidha katika miradi midogomidogo ya miundombinu iliyopewa kipaombele ni ujenzi wa madarasa, mabweni,vituo vya afya,vyoo, vyumba za wauguzi na walimu ambapo vilitegemea na uhitaji wa jamii husika.Ajira za umma katika jamii hizi zilitokana na ushirikishwaji wa wananchi katika ujenzi wa miradi mbalimbali hasa za ujenzi wa barabara,mabwawa,uwekaji wa matuta na upandaji miti.
Jumla ya miradi midogomidogo 51 imeshaanzishwa na kaya 933 zilizowakilishwa na wanaume zimenufaika na kaya 6,583 zilizowakilishwa na wanawake zilinufaika pia.
Kuna faida nyingi ambazo zimepatikana katika mradi huu wa OPEC III nazo ni;
Mbali na mradi huu kuwa na mafanikio makubwa kwa Mkoa wa Arusha, bado kuna baadhi ya changamoto zilizojitokeza wakati wa mradi ukiendelea, nazao ni;
Hata hivyo, baada ya Changamoto hizi kujitokeza Mkoa uliamua kuchukua hatua zifuatazo katika kuhakikisha mradi huu unawafikia walengwa na kwa wakati.
Hitimisho,miradi hii imeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ushirikiano uliokuwepo baina ya Mkoa, Wilaya na wadau mbalimbali wa mradi huu.Mkoa utaendelea kushirikiana na wadau wote wa mradi huu ilikuhakikisha mradi wa OPEC III unafika kila kijiji na kukamilika kwa wakati huku Mkoa ukiendelea kusimamia kwa umakini zaidi.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa