Mkoa wa Arusha ni moja kati ya Mikoa 26 ya Tanzania Bara, wenye ukubwa wa KM za mraba 34,515.5.Kiutawala Mkoa unao Wilaya 6 na Halmashauri 7,Tarafa 23,Kata 33,Vijiji 393,Mitaa 154 na Vitongoji 1471.
Idadi ya watu kwa ongezeko la 2.7% kwa mwaka na inakadiriwa kufikia jumla ya watu wapatao 1,835,787 ambapo wanawake wakiwa sawa na 51.5% na wanaume 48.5%
Mkoa wa Arusha umepakana na Mkoa wa Manyara kwa upande wa Kusini, upande wa Mashariki umepakana na Mkoa wa Kilimanjaro, kwa upande wa Kaskazini umepakana na Nchi ya Kenya na kwa upande wa Magharibi umepakana na Mkoa wa Simiyu na Mara.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa