MAJUKUMU YA KITENGO CHA MANUNUZI
Kutokana na Muundo wa Sekretariati za Mikoa pamoja na Sheria namba 7 ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za toleo namba GN. 446 ya 20/12/2013, majukumu ya kitengo cha manunuzi yameainishwa kama ifuatavyo:-
Kusimamia shuguli za taasisi nunuzi ( Sekretarieti ya Mkoa, hospitali yaMkoa na Wilaya kwa ujumla) ikiwemo manunuzi ya vifaa, huduma na ujenzi kwa njia sahihi zilizo idhinishwa kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013
Kuandaa mpango wa manunuzi wa Mkoa na kupitia mipango ya manunuzi ya Halmashauri za Wilaya zote kama imeandaliwa kwa mujibu wa miongozo ya PPRA (standard documents).
Kusaidia kazi za Bodi ya Zabuni.
Kutekeleza maamuzi na maelekezo ya Bodi ya Zabuni.
Kuwa sekretariet katika vikao vya Bodi ya Zabuni.
Kuandaa nyaraka za zabuni kwa mujibu wa miongozo ya PPRA.
Kuandaa matangazo ya Zabuni.
Kuandaa mikataba ya Zabuni ya Sekretarieti ya Mkoa, hospitali ya Mkoa na pia kupitia mikataba ya manunuzi ya Halmashauri iliyo andaliwa kwa kufuata miongozo ya PPRA.
Kutunza kumbukumbu za michakato ya manunuzi na ufutaji wa vifaa vilivyoisha muda wake (disposal of asset).
Kuandaa na kutunza rejista ya mikataba iliyo sainiwa baina ya Mkoa na wadau wa manunuzi.
MAFANIKIO:
Kitengo cha kusimamia manunuzi kimeonesha mafanikio makubwa katika kutoa ushauri wa kitaalam wa masuala ya manunuzi katika ngazi ya Mkoa na Wilaya, mafanikio katika kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na taratibu za ununuzi wa Umma kwanzia sheria namba 21 ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2005 mpaka sasa kinatekeleza majukumu kwa kuzingatia sheria namba 7 ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013 ambazo zimefanyiwa marekebisho mwaka 2016.
Mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mkubwa wa Seksheni mbalimbali na Vitengo katika Sekretariet ya Mkoa kwani wamekuwa makini katika kutekeleza masuala ya manunuzi kwa kuzingatia sheria na taratibu.
Mafanikio ya kitengo pia hupimwa na kaguzi mbalimbali zinazoendeshwa na Mamlaka ya kudhibiti na kusimamia manunuzi ya Umma, kwani katika vipindi tofauti kuanzia mwaka 2006/2007, 2008/2009, 2011/2012, 2014/2015 wamekuwa wakifanya ukaguzi katika Mkoa wa Arusha na kutoa matokea ya utendaji kazi katika masuala ya manunuzi ya Umma kwa kutumia viashiria mbalimbali (indicators).
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa