Waendesha bodaboda mkoani Arusha wapewa miezi mitatu kuhakikisha wanajifunza sheria na taratibu za barabara bila kusumbuliwa na polisi wa barabarani.
Akitoa kauli hiyo,Waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa Mwigulu Nchemba katika kikao chake na waendesha bodaboda wa mkoa wa Arusha alipokuwa akiwagawia kadi za umili wa bodaboda kwa madereva 107 waliofanikiwa kumaliza mkopo wa mradi wakukopesha pikipiki ulioanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kauli hiyo imetolewa na mheshimiwa waziri baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutoa ombi maalum kwake lakuwaruhusu madereva bodaboda hao kujifunza sheria kwanza kisha ndio polisi waanze utaratibu wakuwakamata wale wote watakaokuwa wamekiuka sheria za barabarani.
Mwigulu Nchemba amewasihi bodaboda wote nchini kuchukulia hii kazi kama yenye heshima ili iweze kuwabadilisha maisha yao na tegemeze wao.
Aidha,amesisitiza utoaji wa leseni kwa bodaboda utazingatia kwa wale ambao watakuwa wanamiliki kofia mbele na hata akiwa na cheti pia atapatiwa leseni,pia abiria atakaekaidi kuvaa kofia basi atapatiwa adhabu yeye nasio dereva kama ilivyokuwa awali.
Akichangia zaidi juu ya mradi huu,Mwiguli Nchemba atachangia kiasi cha shilingi milioni 10 ilikusaidia vijana wengine waweze kukopeshwa pikipiki kwa wingi.
Pia, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,amewaambia bodaboda kuwa wanaweza kutumika katika kubeba watalii ikiwa tu wataweza kufuata sheria na taratibu za barabarani.
Amewapongeza watendaji kata na maafisa tarafa wa Jiji la Arusha kwakuonyesha ushirkiano mkubwa katika kufanikisha makusanyo na kwa wakati, na kiasi cha shilingi milioni 306 tayari zimesharudishwa na milioni 200 zitatumika kukopesha wamama wajasiriamali wadogo kwa mkopo wa shilingi laki 2 kwa wamama 500.
Amesema kiasi cha pesa kinachobaki cha zaidi ya milioni 100 kitatumika kukopesha waendesha bodaboda wengine,hii itasaidia kuwawezesha vijana wengi kumuliki pikipiki zao wenyewe badala yakutegemea pikipiki za watu wengine ambazo zinawabana sana.
Kamanda wa polisi kitengo cha barabarani Joseph Buberwa,amewataka bodaboda kuhakikisha wanatii sheria bila shuruti,wapunguze spidi barabarani hususani kwenye makazi ya watu.
Amesema kuwa polisi barabarani hawatawakamata bodaboda ambao hawana leseni lakini wana cheti cha udereva na watawapa mda wakuhakikisha wanapata lesenina amewapongeza madereva 250 waliofanikiwa kuhitimu mafunzo ya udereva.
Akisisitiza zaidi mwenyekiti waumoja wa madereva bodaboda (UBOJA) bwana Mauridi Makongoro,amesema mradi huo umewanufaisha sana bodaboda wengi kwani umewatoa katika mazingira yakuendesha bodaboda za watu wengine na sasa wanamiliki zao wenyewe na wameweza kuingiza kipato chakutosha.
Mradi huu ulianzishwa mwaka 2017 na mheshimiwa Gambo kwa lengo lakuwakwamua bodaboda wa Jiji la Arusha katika changamoto yakukosa mtaji wakumiliki pikipiki zao, vijana 200 walifanikiwa kukopeshwa pikipiki hizo na kati yao 107 wamemaliza mkopo nakukabidhiwakadi za umiliki wa pikipiki na wengine wanaendelea na marejesho.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa