• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

AHADI YA MAKAMU WA RAIS YATIMIA KETUMBEINE;WAPATA GARI LA WAGONJWA

Posted on: March 4th, 2024


Na Elinipa Lupembe


Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa, ile ahadi aliyoitoa Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kwa wananchi wa Tarafa ya Ketumbeine, ya kuwapa gari la wagonjwa wa dharura (ambulance) leo imetimia.


Dkt. Mpango ametimiza ahadi hiyo aliyoitoa, kufuatia ombi la wananchi wa Ketumbeine, wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Longido ya kuzindua Kituo cha Afya Ketumbeine Februari 10, 2024.


Wakizungumza wakati wa  kukabidhiwa gari hilo, na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Loy Thomas Ole Sabaya, wananchi hao wameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwajali na kuwapa kipaumbele,  miradi mingi ya maendeleo ikitekelezwa kwenye maeneo yao, ikiwemo kituo hicho kioya cha Afya.


Diwani wa kata ya KetumbeineMhe. Timotheo Menyoriti Laizer, licha ya kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuwajengea kituo hicho cha afya, haikutosha na kuwaletea gari la wagonjwa, ambalo litaenda kuondoa vifo visivyo vya lazima kwa wakazi wa Ketumbeine, hususani vifo vya kinamama wajawazito na watoto, ambao walikuwa kwenye hatari kubwa ya kupoteza maisha kwa kucheleweshwa kupata huduma.


"Kipekee tunamshukuru Dkt. Mpango kwa kutimiza ahadi yake kwa wakati, inatupa mwanga ni kiongozi wa kipekee anayethamini watu, pia tunamshukuru Mama Samia kwa kuwajali wananchi wake, kwa kipindi kifupi cha uongozi wake Ketumbeine tumepata miradi mingi ya maendeleo, miradi ambayo imepunguza kero na changamoto nyingi za wananchi, ambapo hapo awali walikuwa kama wametengwa" Mhe. Menyoriti.


Naye, Noa Keiyan Mollell mkazi wa Ketumbeine, amemshukuru pia Mhe. Rais na kusema kuwa hapo awali, walitumia punda kubeba wagonjwa pindi wanapozidiwa lakini sasa wamepata gari, jambo ambalo, wanaiona Serikali ya Mama Samia ni ya tofauti sana, inayowajali na kuwapenda sana wananchi wake.


Mariam Laizer, amesema hatujawahi kuona maendeleo ya kasi hii, tunamshukuru mama Samia kwa kuwajali wanawake wa Ketumbeine, kwa kuleta huduma ya upasuaji kwenye kituo cha afya, zamani walilazimika kwenda Longido kufanyiwa upasuaji lakini sasa huduma zote zinapatikana kituoni hapo.


"Tunamshukuru mama Samia, wajawazito walipoteza watoto na wengine walipoteza maisha kwa kuchelewa kupata huduma, kwa kutupa gari hili, mama ametuletea uzima, ametuponya maumivu yote ya kupoteza ndugu zetu kwa kukosa huduma" Amesema Mariam


Hata hivyo Mganga Mkuu wa wilaya ya Longido, Dkt. Methew Majan, amesema kuwa, uwepo wa gari la wagonjwa kituoni hapo,  utarahisisha usafiri pindi wanapotokea wagonjwa wa dharura, kwa kuwa hapo awali walilazimika kusubiri gari kutoka hospitali ya wilaya zaidi ya Km 55.


#arushafurasalukuki 




                        
                       
                        </div>
                        <!-- /.right-sidebar-content -->
                        <!--/END RIGHT SIDEBAR CONTENTE SECTION-->
                    </div>



<div class=

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa