Mkoa wa Arusha umeshika nasafi ya 7 Katika ongezeko la pato la taifa na nafasi ya 6 kwa pato la mtu mmoja mmoja.
Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Hassan Kimanta,amesema ni jambo lakujivinia sana kwa mkoa wetu wa Arusha na jitiada zaidi zinaitaji ilikuweza kushika nafasi zajuu zaidi.
Ameyasema yaho katika kikoa cha ushauri cha mkoa (RCC) nakuhimiza halmshauri zote zinatakiwa kuongeza fursa zaidi za mapato ili kuweza kuboresha mapato.
“Tunaweza kuongeza nguvu zaidi kupitia halmashauri zetu natukaweza kuongeza mapato ambayo yatatusaidia kuongeza pato la taifa kwa ujumla”.
Mkoa bado utaendelea kusimamia matumizi sahihi ya fedha zote za halmashauri na pia kusimamia miradi yote ya maendeleo na kuhakikisha wananchi wananufaika nayo nakuleta maendeleo kwenye maeneo yao.
Aidha,amesema mkoa utaendelea kuhamasisha wananchi wajikite zaidi kwenye shughuli zakujenga uchumi wa mkoa na nchi kwa ujumla.
Kikao cha ushauri cha mkoa kilikuwa maalum kwaajiri yakupitisha bajeti ya mkoa kwa mwaka wa fedha 2018-2019.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa