Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema Mkoa wa Arusha umeshika nafasi ya pili Kitaifa katika afua za lishe.
Ameyasema hayo alipokuwa akiwasainisha mikataba ya Lishe Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmshauri za Mkoa wa Arusha.
"Tumejitaidi kufanya vizuri katika kukidhi vigezo vya lishe sasa twendeni tukaweke nguvu zaidi katika kusimamia afua za lishe ili tuweze kuongoza".
Swala la lishe likawe agenda ya kudumu kwa ngazi za Wilaya na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi lisimamieni hili.
Timu ya afya ikafanye kazi ya kutoa elimu na hamasa hadi ngazi za vijiji ili wananchi wapate uwele zaidi.
Kukosa lishe nikusababisha umaskini katika Taifa kwani hakutakuwa na Jamii inayoweza kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii kwasababu wengi watakuwa na utapiamlo.
Nae, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Musa amezitaka halmashauri kutoa fedha za lishe kwa kila robo mwaka na mapema ili kurahisisha shughuli za lishe kufanyika kwa wakati.
Aidha, amewataka wataalamu wa lishe kufanya ukaguzi wa vyakula katika mashule ili kujihakikishia kuwa chakula kinachotolewa kwa wanafunzi kinafaa.
Kikao cha kusaini mikataba ya lishe kwa Mkoa wa Arusha kilijumuisha kamati za ulinzi na usalama Mkoa, Wilaya, Wakurugenzi, na Makatibu Tawala wa Wilaya ambapo Kitaifa Mkataba huo ulisainiwa na Mhe.Samia Suluhu na Wakuu wa Mkoa mnao septamba 30, Jijini Dodoma.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa