• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

ASILIMIA 95.38 YA VIJIJI VYOTE VYA MKOA WA ARUSHA VIMEFIKIWA NA UMEME WA REA..

Posted on: November 26th, 2023

Na Elinipa Lupembe.


Vijiji 351 vya mkoa wa Arusha, sawa na asilimia 95.38 vimefikiwa na miundombinu ya umeme, huku wakandarasi wakiendelea na kazi ya kukamilisha usambazaji wa umeme kwenye vijiji 17 vilivyosalia ili kukamilisha vijiji vyote 368 vya mkoa huo na kufikia asilimia 100.


Hayo yamethibitishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, alipopata fursa ya kuzungumza, muda mfupi kabla ya kumkaribisha, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, alipotembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusafirisha Umeme cha Lemuguru - mkoani Arusha.


Mhe. Mongella, kwa niaba ya wananchi wa mkoa huo,  ameishukuru Wizara ya Nishati na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuijali Arusha, kwa kutoa  fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo huku ikitoa kipaumbele kwa kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu ya umeme kupitia mradi wa umeme vijijini (REA), miradi ambayo  iko hatua za ukamilishaji na kuvifikia vijiji vyote 368 vya mkoa wa Arusha.


"Kwa sasa Mkoa wa Arusha unakamilisha ufungaji wa umeme kwenye vijiji 17 vilivyosalia, huku wakandarasi wakijikita katika kuendelea kusambaza umeme kwenye vitongoji na kuwafikia watumiaji, jambo ambalo linachochea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake" Ameweka wazi RC Mongella


Ameongeza kuwa matokeo ya uwepo wa umeme Arusha, yameanza kuonekana wazi, kupitia  mabadiliko katika pato la wananchi sio kwa kuwaka tuu, bali kukuza uchumi wa mkoa, huku uanziashwaji wa viwanda vidogo ukiendelea, na wananchi kulazimika kujikita katika shughuli za uzalishaji, shughuli zinazosababisha, uwepo wa amani na utulivu katika mkoa huo.


"Nikiri wazi kuwa, wananchi wa Arusha wamenufaika na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, huku Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 - 2025, ikitekelezwa kwa asilimia 100 na kufikia lengo la serikali la kuhakikisha huduma za Umeme,  zinawafikia wananchi kwenye maeneo yao hususani wananchi waishio vijijini" Amethibitisha Mhe. Mongella.


Awali mradi wa Kituo cha Umeme Lemuguru, unatekelzwa na serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 14.295, ukiwa umefika asilimia 30 na unategemea kuhusambaza na  kuongeza upatikanaji wa huduma za umeme kwa  wananchi wa maeneo ya Longido, Monduli, Arumeru pamoja na Jiji la Arusha.

#ArushaFursaLukuki



Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa