Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Amir Mohamed Mkalipa mapema asubuhi ya leo Novemba 27, 2024, ametumia haki yake ya kikatiba kupiga Kura kwenye kituo cha shule ya Msingi Kilimani kitongoji cha Magadirisho kuwzchagua viongozi wake wa Serikali ya Mtaa.
Mhe.Mkalipa awewasisitiza wannachi wote waliojiandikisha kujitokeza kupiga kura kwenye maendeo yao huku akiwahakikishia hali ya maeneo yote kuwa ni tulivu na salama.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewapongeza wasimamizi wa Vituo kwa kufungua vituo kwa mapema kwa kuzingatia muda ulioelekezwa, na kuwzhakikishia wananchi kura zitahesabiwa kwa haki na wananchi kupata viongozi wao
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa