Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Salum Kalli hakuwa nyuma bali, amewaongoza wanannchi wa wilaya hiyo kwa kuwa wa kwanza kujiandikisha kwenye daftari la mkazi, ili kupata sifa ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
Mhe. Kalli amewataka wananchi wote kufika kwenye vituo teule vilivyoainishwa na serikali kwa ajili ya zoezi hilo, muhimu lenye lengo la kuwapa wananchi sifa ya kupiga kura na kuchagua viongozi wao wa vijiji na vitongoji ifikapo Novemba 27,2024.
Amesisistiza kuwa, kila mwananchi wa Longido anao wajibu na haki ya kushiriki cuhaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kujiandikisha na kuweka wazi kuwa, vituo vyote vitakuwa wazi kuanzia saa 02:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni, kuanzia tarehe 11 hadi tarehe 20 Oktoba, 2024.
"Ninawahimiza wananchi wote wenye umri wa kuanzia miaka 18, kushiriki kikamilifu katika zoezi hili ili kutimiza haki yao ya kidemokrasia na kuhakikisha wanapata fursa ya kuchagua viongozi wanaowakilisha maslahi yao kwenye serikali za mitaa".Amesema Mhe.Kalli
"SERIKALI ZA MITAA SAUTI YA WANANCHI JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI"
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa