Mkuu Wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Amir Mohamed Mkalipa amefungua rasmi Tamasha la kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka huu Tarehe 27 Novemba 2024, lililofanyika Septemba 21, 2024, lililofanyika kwenye viwanja vya Ngareselo halmashauri ya Meru, mkoa wa Arusha
Mhe. Mkalipa katika Tamasha hilo amewataka wananchi wote wa Halmashauri hiyo kujitokeza tarehe 11 hadi 20 mwezi Oktoba, 2024 kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura pamoja na kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa ifikapo mwezi Novemba 2024.
Ameeleza kuwa GN kwa maana ya mikapa ya maeneo imeshatangazwa na vituo vya kupigia kura vimeshatambuliwa na kubandikwa kwenye Kata, Vitongoji na Vijiji.
Pia, Mkalipa ameeleza kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 utakuwa ni uchaguzi wa Haki na Amani hivyo wananchi wahakikishe wanajitokeza kujiandikisha.
" Kati ya sifa za mwananchi kumwezesha kuweza kupiga kura lazima awe na sifa zilizoainishwa ikiwa ni pamoja na kuwa mwananchi huyo awe amefikisha miaka 18, awe Raia wa Tanzania lakini awe Mkazi wa Eneo husika" amesema Mkalipa
Mwisho Mhe. Mkalipa ameeleza kuwa suala la kuhamasisha uchaguzi ni suala la kila mtanzania hivyo wananchi wote wachukue jukumu la kuhamasisha suala la uchaguzi wa serikali za Mitaa
Tamasha hilo lililofanyika katika Viwanja vya Ngarasero Kata ya Usariver likiambatana na michezo mbalimbali kama Matembeze ( Jogging), mpira wa Miguu, kukimbiza kuku, kukimbia na yai na michezo mingine.Tamasha hilo limepewa jina la KIMBIA KIUCHAGUZI NA MERU DC.
Kauli Mbiu " Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitoteke kushiriki Uchaguzi"
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa