• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

DC NG'UMBI AKIRI KWA SASA LONGIDO NI SHWARI; KAZI INAENDELEA

Posted on: November 7th, 2023

Na Elinipa Lupembe.


Mkuu wa wilaya ya Longido Mhe. Marco Ng'umbi amesema kuwa, hali ya wilaya ya Longido kwa sasa ni shwari, hali inayoruhusu wananchi wake kujikita zaidi kwenye shughuli za kiuchumi na kijamii zinazoongeza hali ya uzalishaji mali walayani humo.


Akizungumza wakati wa mkutano na Mkuu wa mkoa wa Arusha mara baada ya kuwasili wilayani hapo, Mhe. Ng'umbi amethibitisha hali ya utulivu katika wilaya hiyo, huku wananchi wake wakiwa msatri wa mbele kulitumikia Taifa lao.


Ameongeza kuwa, viongozi na watalamu nao wanaendelea vema kutekeleza majukumu yao, kwa kusimamia shughuli zote hususani katika usimamizi wa miradi ya maendeleo kisekta, huku wakiwa mstari wa mbele kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 - 2025.


Mhe. Ng'umbi ameweka wazi kuwa serikali imetoa fedha za kutekeleza miradi ya elimu msingi na sekondari ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya za sekondari wasichana, kwa gahrama ya bilioni 3, ujenzi wa mabweni mawili ya wavulana na uzio shule ya sekondari Longido pamoja na ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kamweni Mirasi na zote ziko katika hatua nzuri za utekelezaji.


Kwa upande wa miundombinu ya barabara, ameweka wazi kuwa barabara kuu zote zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka licha ya changamoto zinazojitokeza kutokana na mvua zinazoendelea lakini TANROAD NA TARURA,  wanaendelea kufanya matengenezo ya muda maalum pamoja na kuchunguza maeneo  hatarishi na kuyafanyia kazi kwa wakati.


Hata hivyo upande wa Umeme,  vijiji vyote vya wilaya ya Longido vimefikiwa na miundombinu ya umeme na serikali kuendelea na kasi ya kufikisha umeme kwenye vitongoji na hatimaye kuwafikia wateja wa nyumba kwa nyumba.


Aidha, huduma za afya zinaendela kuimarika,  zahanati zimejengwa kwenye maeneo ya pembezoni huku kituo cha afya cha Ngarnaiboru na  Longido vyote vinatoa huduma za afya kwa wananchi huku Serikali ikileta dawa na vifaa tiba pamoja na wahudumu wa afya katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya na kuongeza kuwa ifikapo 2025, hali ya utoaji wa huduma itakuwa imeimarika zaidi.


Awali ameweka wazi kuwa, huduma ya maji vijijini nazo zinaendelea kuimarika licha ya kuwa bado kuna changamoto kwa baadhi ya miradi ikiwemo mradi wa Tinga tinga na Ngeleani, mi4adi amabyo mkandarasi anasuasua  na mpaka sasa ametuchelewesha kwa zaidi ya miezi 6 jambo ambalo litasababisha mradi huo kushindwa kukamilika mwezi Aprili kamailivyokusudiwa.


Hata hivyo ametumia wasaa huo kuishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kaiz kubwa anayoifanya ya kuhakikisha huduma za jamii licha ya kuimarika zinawafikia wananchi katika maeneo yao.


"Wilaya ya Longido ni moja ya wilaya za pembezoni mwa nchi, serikali ya awamu ya sita imetoa fedha nyingi za kutekeleza mirafi kisekta, miradi ambayo imewafikia na kuwanufaisha wananchi ambao hapo awali walionekana kutelekezwa, kwa sasa Longido ni shwari, kila mwanaLongido anajisikia na yeye ni Mtanzania halali" Amebainisha Mhe. Ng'umbi.

#ArushaFursaLukuki

#KaziInaendelea

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa