Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Meru, Mwi. Zainabu Makwinya, akiwasilisha taarifa fupi ya ya mradi wa upanuzi na ukarabati wa Hospitali ya wilaya ya Meru, mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kwenye kikao kifupi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha leo Machi 13, 2024.
Mkurugenzi huyo, ameielezea Kamati kuwa, halmashauri ya Meru, imepokea fedha kiasi cha shilingi milioni 900 kutoka Serikali Kuu, kwa ajili ya upanuzi na ukarabati wa Hospitali hiyo ya wilaya na tayari utekelezaji wa mradi huo umeanza na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Aprili, 2024.
Amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kitajumuisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo Maabara, jengo la Famasi, Kichomea taka pamoja na ukarabati wa wodi ya watoto.
Amefafanua kuwa, jengo la wagonjwa wa nje litagharimu shilingi milioni 385.2, milioni 231.9 zitajenga jengo la maabara, milioni 168.8 jengo la famasi, kichomea taka kitagharimu milioni 80 huku milioni 33 zikikarabati wodi ya watoto hospitalini hapo.
Awali, Wajumbe hao wa Kamati, wakiongoza na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Denis Lazaro Londo (MB), wako mkoani Arusha kwa ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Maendeleo halmashauri ya Arusha, Meru na Longido.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa