• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

DKT. MPANGO AZISHAURI SERIKALI ZA AFRIKA KUWAPA UHURU WAKAGUZI WA NDANI..

Posted on: April 17th, 2024

DKT. MPANGO AZISHAURI SERIKALI ZA AFRIKA KUWAPA UHURU WAKAGUZI WA NDANI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amezishauri  Serikali za nchi za Afrika kuwa na Sera na Sheria zitakazowapa uhuru kwa wakaguzi wa ndani kufanya kazi yao kwa uhuru na kutoa ushauri wenye uhalisia.

Dkt.Mpango ametoa ushauri huo, wakati akifungua Mkutano wa 10 wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) na kusema kuwa,  serikali za Afrika zinapaswa kuwa na kifungu katika Sheria ya Ukaguzi wa Umma ambacho kitawapa nguvu na kuwalinda Wakaguzi wa Ndani dhidi ya ushawishi na kuingiliwa katika majukumu yao isivyostahili.

Amefafanua kuwa, mfumo wa kisheria unaweza pia kuanzisha uhusiano katika utoaji taarifa za kiutendaji na kiutawala kwa wakaguzi wa ndani kwa kuzingatia Mfumo wa Kimataifa wa Mazoezi ya Kitaalamu (IPPF), kama suluhu ya uwezekano wa vitisho na vikwazo kutoka kwa baadhi ya Wakurugenzi Wakuu katika taasisi zao.

Aidha, Dkt. Mpango amesisitiza umuhimu wa Serikali, Wakuu wa Mashirika ya Umma na Binafsi kutenga bajeti sahihi za mafunzo kwaajili ya vijana wataalamu wa Ukaguzi wa ndani ili kuwajengea uwezo zaidi katika utaalamu wao kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika ukaguzi wa ndani na kutafuta njia sahihi za kuzitatua.

Halikadhalika Makamu wa Rais amesema kutokana na maendeleo ya kasi ya teknolojia hususani matumizi ya akili mnemba (AI) Wakaguzi wa Ndani wanahitaji kujipatia ujuzi wa hali ya juu zaidi wa kiteknolojia ili kuwawezesha kugundua, kuangalia na kudhibiti ukiukwaji wa taratibu. Amesema Wakaguzi wa Ndani wanapaswa kuendana na maendeleo ya haraka ya kiteknolojia, kurejea mifumo ya usimamizi wa taarifa, miundo ya uendeshaji na mikakati ya biashara ili kukabiliana na ongezeko la ukosefu wa usalama wa mtandao.

Pia Makamu wa Rais amewasihi Wakaguzi wa Ndani wote kuona wajibu wa kutekeleza majukumu yao kwa kutumia kanuni na viwango vya kimataifa. Amezihimiza Serikali za Afrika na Wadau kutoa msukumo wa kuidhinishwa kwa Wakaguzi wa Ndani kama ilivyo utaratibu wa kawaida katika taaluma zingine.

@dr_philip_isdor_mpango @afiia_africa3618



Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa