Na Elinipa Lupembe - Arusha
Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango amefika kwenye msiba wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Tixon Nzunda, licha ya kusaini kitabu cha Maombolezo ametoa salam za pole kwa niaba ya Serikali, mapema leo Juni 19, 2024 Moshi Kilimanjaro.
Akitoa salamu za hizo, Mhe. Dkt.Mpango amemuelezea marehemu Dkt. Tixson kuwa, alikuwa ni mtumishi muadilifu wakati wote wa utumishi wake ambaye mara zote, alimtanguliza hofu ya Mungu, katika kuwatumikia wanancmfa jambo ambalo watumkwetuwa Umma wanapaswa kuiga mfano wake huku akisistiza kuacha pengo na alama kubwa sana katika utumishi wa Umma.
"Binafsi nimefanya nae kazi sana nikiwa Waziri wa fedha na yeye akiwa ofisi ya Waziri Mkuu, mara kwa mara tulikuwa tukifanya vikao vyetu vya utatu na watumishi, Tixson alikuwa mtu makini na mpole sana , tukio hili limetuumiza sana sisi kama Serikali"
Aidha ametumia wasaa huo, kuwapongeza wananchi wa Kilimanjaro wakiongozwa na Mkuu wao wa Mkoa Mhe. Nurdin Babu kwa ushirikano mkubwa tangu kutokea kwa msiba huo, na kutoa pole kwa familia, ndugu jamaa na marafiki pamoja na watanzania wote walioguswa na msiba huo na kuwataka kuendelea kushirikiana na kujifunza kuzihesabu siku zetu kwa kuishi vizuri na kila mtu katika kazi, majirani na jamii ili siku moja uweze kuhadithiwa vizuri.
Awali Marehemu Dkt. Nzunda, alifariki dunia kufuatia ajali ya gari na dereva wakiwa njia kuelekea kiwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kwa ajli ya kumpokea Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango.
Marehemu Dk. Nzunda na dereva wake, walipoteza maisha mara baada ya gari aina ya VXR, kugongana uso kwa uso na lori la kubeba nishati ya gesi safi, mali ya Kampuni ya Orange Gas, lenye namba za usajili T 655 ABY, aina ya Scania lililokuwa likitokea Arusha kuelekea Moshi.
Bwana ametoa Bwana ametwaa Jina lake Lihimidiwe
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa