Kaimu katibu tawala wa Mkoa wa Arusha bwana David Lyamongi, amewataka waratibu wa uwandikishaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5 kuendelea kuhamisha wananchi wajitokeze zaidi hata baada ya kampeni hiyo.
Ameyasema hayo alipokuwa akitembelea vituo vya uwandikishaji vya Mkoa wa Arusha kwa lengo la kujionea namna zoezi hilo likiendelea baada ya uzinduzi uliofanyika Mei 12, 2021, kwa Mikoa ya Arusha na Manyara Jijini Arusha.
Amesema zoezi hilo lilikuwa na lengo la kuhamasisha wananchi kupata vyeti vya Watoto wao walio chini ya miaka 5 kwani ni kundi ambalo lilikuwa limesahaulika sana.
Aidha, bwana Lymongi amesema kwa Sasa vyeti hivyo ni moja ya utambulisho vya Mtanzania katika maeneo mbalimbali ya nchi, hivyo ni vizuri kila rika likapata cheti hicho.
Akifafanua zaidi mratibu wa uwandikishaji Watoto chini ya miaka 5 Mkoa wa Arusha bwana Denis Mgiye, amesema hata kampeni hiyo ya uwandikishaji kwa siku 90 ikiisha nguvu kubwa itapelekwa kwa watoto wanaozaliwa wapatiwe vyeti ndani ya siku chache.
Kampeni ya uwandikishaji vyeti vya Watoto chini ya miaka mitano ilizinduliwa rasmi Mkoani Arusha Mei 12,2012.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa