Watumishi wa umma wametakiwa kufanyakazi kwa uadilifu, uzalendo na uwajibikaji katika kutoa huduma kwa wananchi.
Yamesemwa hayo na Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais,Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza na watumishi wa Umma kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Jiji la Arusha katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Amesema kuna ulazima wa kuweka mikakati sahihi kwa wakati sahihi ili iweze kuleta tija katika utendaji kazi.
Amesisitiza zaidi usimamizi wa miradi ya maendeleo ili iweze kuleta tija na thamani yake iendane na fedha zilizotolewa.
Pia, usimamizi wa fedha za TASAF kwa walengwa zikasimamiwe ili wakatumie kwa manufaa zaidi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella Mkuu wa Wilaya ya Arusha Said Mtanda amesema maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri anaenda kuyasimamia kwa kushirikiana na viongozi wengine katika ngazi za halmashauri ili yalete ufanisi mkubwa zaidi.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa