Jumuiya ya Maridhiano na Amani nchini Tanzania (JMAT) leo Februari 12, 2025 Jijini Arusha, wamezindua shamrashamra mbalimbali kuelekea kwenye Kilele cha "Maridhiano Day" ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika Jijini Arusha kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC chini ya Kaulimbiu isemayo "Uchaguzi wa amani 2025 kwa maendeleo ya watanzania wote."
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa New Safari Hotel Jijini Arusha amekuwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) Sheikh Alhad Mussa Salum ambaye aliambatana na Mgeni maalum, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda.
Kulingana na Shekh Dkt. Alhad, Kuelekea Kilele Februari 26,Shughuli mbalimbali zitafanyika Jijini Arusha zikiongozwa na Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini na Viongozi wa kimila ikiwa ni pamoja na Kuchangia damu kufanya utalii wa ndani, Michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu utakaowahusisha Viongozi wa dini na wana jamii, kutembelea wafungwa Jijini Arusha pamoja na mengineyo.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa