"Wakuu wa Wilaya nendeni mkafanye vikao na mawakala wa Barabara ( TANROAD na TARURA) ili kuwe na uwelewa wa pamoja kuhusi miradi ya Wilaya husika".
Maelekezo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella alipokuwa akifungua kikao cha Barabara cha Mkoa wa Arusha.
Changamoto ya vikao hivi, viongozi wengi wa wilaya na Halmashauri mnakutana na taarifa zenu hapa kwenye kikao cha Mkoa na mambo mengi yanakuwa mageni kwenu.
Mongella amesisitiza zaidi kwa viongozi hao kuhakikisha wanajadili miradi yao kwanza na kupitia taarifa zote kabla hazijaletwa kwenye vikao ngazi ya Mkoa.
" Kwa kufanya hivyo inasaidia kujenga uwelewa wa pamoja na kumiliki taarifa hizo".
Mbunge wa Arumeru Magharibi Mhe.Noah Nembrisi amependekeza kwa wakandarasi wanaopewa kazi za ujenzi wa Barabara lazima wawe na uwezo wa kutosha katika kazi hizo ili ziweze kukamilika kwa wakati.
Kikao cha Barabara Mkoa wa Arusha ni kikao cha 45 kwa robo ya 3 mwaka 2021/2022.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa