• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

KAMATI YA BUNGE OR - TAMISEMI YAAGIZA KUJENGWA UZIO VITUO VYOTE VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

Posted on: March 14th, 2024


Na Elinipa Lupembe 


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imemuagiza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, kuweka mpango mkakati wa kujenga uzio kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za Afya Nchini.


Agizo hilo lilekuja kufuatia ombi la wananchi wakazi wa kata ya Olturumet halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, kuiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kujenga uzio kwenye hopitali yao ya wilaya ya Olturumet, ili kuongeza usalama wa wagonjwa na mali za hospitali, wakati  Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa hospitali ya Olturumet, mradi unaotekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 900.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Justine Nyamoga (MB), ameitaka Ofisi ya Rais TAMISEMI kujenga uzio kwenye hospitali hiyo ya Olturumet lakini kuweka mpango endelevu wa kujenga uzio kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini. 


 "Kutokana na umuhimu wa kuongeza usalama wa wagonjwa, mindombinu, mifumo na mali zote kwenye  vituo vya kutolea huduma za Afya nchini, ni vema Ofisi ya Rais TAMISEMI ikaweka mpango endelevu wa kujenga uzio, ambao utazuia na kuepusha changamoto mbalimbali zinazoweza kuepukika" Amesema Mhe. Nyamoga.


Awali akizungumza kwa niaba wananchi, Diwani wa kata ya Olturumet Mhe. Joseph Tinayo, ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha nyingi zilizotekeleza miradi kwenye kata hiyo, ikiwemo shilingi milioni 900 za mradi huo wa upanuzi wa hospitali unaojumuisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la Maabara, Mionzi na jengo la kuhifadhia maiti na kuiomba serikali kujenga uzio katika hospitali hiyo.


"Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya sita, imefanya kazi kubwa na nzuri, Dkt.Samia ametutendea haki wananchi wa Olturumet, barabara imewekwa lami, majengo yote muhimu yanaongezeka kwa kasi, ombi letu kubwa, hospitali hii ijengwe uzio, ili kuongeza ulinzi na zaidi hadhi ya hospitali yetu" Ameweka wazi Mhe. Tinayo.


Hata hivyo Naibu Kaibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Eng. Rogatus Mativila, amekiri kupokea agizo hilo na kuahidi kulifanyia kazi.


Wajumbe hao wa Kamati, wamefanya ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Maendeleo halmashauri ya Arusha, Meru na Longido.

 #arushafursalukuki




                        
                       
                        </div>
                        <!-- /.right-sidebar-content -->
                        <!--/END RIGHT SIDEBAR CONTENTE SECTION-->
                    </div>



<div class=

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa