• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA YAWASILI MKOANI ARUSHA KUKAGUA MIRADI YA TSCP NA TACTIC...

Posted on: October 13th, 2023

Na Elinipa Luoembe

Kamati ya Kudumu ya Bunge Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, imewasilia mkoani Arusha kwa ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na kwa fedha za uendeshaji wa Mjiji na Majiji nchini ( TSCP).


Wakiwa mkoani Arusha wajumbe hao watatembelea utekelezaji wa mradi wa katika eneo la kuhifadhi taka ngumu 'Dampo' kata ya Muriet pamoja na miundombinu ya barabara kuingia na kutoka Jiji la Arusha.


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge TAMISEMI Mhe. Denis Lazaro Londo (MB) amesema kuwa lengo la  ziara hiyo ni kutembelea miradi ya uboreshaji wa Miji na Majiji ni kujionea maendeleo ya mradi ili kubaini changamoto ikiwa ni maandalizi ya utekelezaji wa mradi mkakati unaokuja wa kuboresha hadhi za Miji na Majiji 'Tanzania Cities Transforming Infastructure & Competitiveness Project' (TACTIC).


"Tumetembelea halmashauri nne ikiwemo za Jiji mbili na Manispaa mbili ambazo ni wanufaika wa mradi wa TSCT ili kufahamu maendeleo yako ikiwa ni mwelekeo wa mradi unaotarajiwa kuanza wa kuboresha hadhi za Miji na Majiji nchini" Amesema Mwenyekiti huyo


Hata hivyo Naibu Waziri  Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi amesema, kupitia mradi wa TSCP kamati itapata uwelewa wa pamoja utakaokuwa dira ya utekelezaji wa mradi wa awamu ya pili wa kuboresha Majiji wa TACTIC kwa kuwa miradi hii ndio miradi ya kimkakati inayofuata baada ya hii kukamilika.


Ameweka wazi kuwa serikali ya awamu ya sita inategemea kuanza awamu ya pili ya kuetekeleza miradi mkakati ya kuboresha Miji na Majiji kwenye halmashauri 12, Jiji la Arusha liwa miongoni mwao kwa ufadhili wa Benki Kuu ya Dunia, ikihusisha ujenzi wa masoko, vituo vya mabasi pamoja na miundombinu ya barabara.


"Moja ya eneo lililopata fedha nyingi  ni Jiji la Arusha, kwa kuwa kila mtu anafahamu idadi kubwa ya wageni wanaoingia na kutoka kupitia Arusha kwa shughuli za utalii, uchumi na uatawala" Amesema Mhe. Ndejembi


Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella licha ya kuwakaribisha wajumbe hao wa Kamati ya Kudumu ya Bunge TAMISEMI na kuwahakikishia usalama wa mkoa wa Arusha amewashukuru kwa kupata fursa ya kupitia utekelezaji wa maendeleo ya Jiji la Arusha kwa kuwa usimamizi wa miradi ndio nyenzo ya maendeleo ya Taifa letu.


Amesema kuwa, kwa sasa kuna uwekezaji mkubwa unaendelea katika mkoa wa Arusha ukihusisha viwanda, kilimo, ufugaji na madini huku utalii ukiwa ndio muhimili wa uchumi wa wananchi wa mkoa huo, na kuongeza kuwa mradi wa TSCP umewezesha uwepo wa miundombinu rafiki unaochochea ukuaji wa kasi wa maendeleo ya kiuchumi.


Aidha amemshukuru Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuhamasisha utalii kupitia Filamu ya Royal Tour, programu ambayo imeleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya utalii ikiwa ndio muhimili wa uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.


"Mradi unaokuja wa kuboresha majiji awamu ya pili (TACTIC) utachangia ukuachi wa uchumi katika sekta zote hususani sekta nyeti ya utalii, mwaka huu msimu wa utalii umeunganisha tunapokea idadi kubwa ya watalii karibu mwaka mzima, mkakati wetu kama mkoa ni kuhimiza uwekezaji katika sekta ya utali kwa kuwa na uhitaji mkuwa wa maeneo ya malazi yatakayokuwa na  hadhi kuwakarimu wageni wanaofika Arusha"Amebainisha Mhe. Mongella


#Arushafursalukuki

#KaziInaendelea








Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa