Wajumbe wa Kamati ya Siasa mkoa wa Arusha, wakiongozwa na Mwenyekiti CCM Mkoa huo, Loy Thomas Sabaya, wametembela na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Lepurko, kata ya Lepurko Tarafa ya Kisongo, ikiwa na ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilaya ya Monduli.
Wajumbe hao wa Kamati ya Siasa wamemuagiza Mkurugenzi Mtendaji kupitia Ofisi ya Mkuu wa mkoa, kukamilisha mradi huo kabla ya mwezi Aprili 30, 2024 ili wanafunzi waweze kuingia shuleni hapo.
Mwenyekiti Sabaya, amesema kuwa, mradi huo uko nyuma ya wakati kulinganisha muda wa utekelezaji wa mradi licha ya changamoto zilizojitokeza na kusababisha ucheleweshwaji wa mradi, ameuagiza uongozi wa wilaya na halmashauri kukamilisha mradi huo ifikapo tarehe 30 Aprili, ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa majengo na samani za madarasa na ofisi.
Hata hivyo, Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe.Festo Shemu Kiswaga, ameahidi kutekelza maagizo hayo kwa kufuatilia na kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa siku hizo zilizoelekezwa.
Akisoma taarifa ya mradi huo, Mkuu wa shule ya sekondari Lopurko Mwl. Sadoth Rutayuga, amesema mradi huo umetekelezwa kwa gharamaya shilingi milioni 602.2, ikiwa milioni 584.2 fedha kupitia mradi wa SEQUIP na milioni 18 ni nguvu za wananchi umetekelezwa kwa shilingi milioni 584.2 Sequip
Mradu huo, umejumuisha ujenzi wa jengo la utawala, vyumba naen vya madarasa, ujenzi wa maabara, maktaba , kisima cha maji matundu ya vyoo kichomea taka, umegharimu milioni 692.2
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa