• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

KAMISHINA MSTAAFU WA UHIFADHI - TANAPA, DKT.  KIJAZI; AAGWA RASMI BAADA YA KUSTAAFU UTUMISHI WA UMMA..

Posted on: November 16th, 2023

Na. Zainabu Ally - Arusha

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) jana tarehe 16.11.2023 limemuaga  rasmi aliyekuwa Kamishina wa Uhifadhi Dkt. Allan Kijazi baada ya kumaliza utumishi wake katika shirika hilo.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini TANAPA Jenerali Mstaafu George Waitara amempongeza Kamishina Mstaafu Dkt. Kijazi kwa kuliletea shirika hilo mageuzi na mafanikio makubwa katika kipindi cha uongozi wake akitaja kuwa ni sehemu ya matokea ya uongozi ulio imara na thabiti.


"Ulishiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko makubwa ya kimfumo ndani ya shirika hususani katika kubadili muundo wa utendaji kutoka wa kiraia na kuwa wa kijeshi, mfumo ambao umeleta ufanisi, nidhamu, uwajibikaji na uzalendo katika utendaji ,hivyo haitakuwa rahisi kuelezea historia ya TANAPA bila kukutaja kwa mchango wako huo mkubwa"


"Kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini TANAPA ninakupongeza sana kwa kustaafu kwa heshima kwani kazi yako ilikuwa ngumu sana hasa katika wakati wa ujangili uliotishia kutoweka kwa wanyama adimu kama vile Faru pamoja na kupambana na uhalifu mwingine ndani ya hifadhi zetu. Pia nakupongeza kwa uvumilivu wako na msimamo uliokuwa hata kama maamuzi ya Bodi ya Wadhamini yalitofautiana na TANAPA ulisimama na kuonesha dira iliyopelekea kupata mwelekeo sahihi.


Akitoa salamu zake za kwa heri Kamishna Mstaafu wa Uhifadhi Dkt. Kijazi aliwashukuru Marais wa awamu zote 3 aliofanya nao kazi na kumpandisha kushika nyadhifa kubwa na muhimu katika Taifa.


"Alisema, kwa upekee sana nawashukuru marais wa awamu zote walioniteua ili kulitumikia Taifa letu, hakika kwangu ni heshima kubwa mnoo lakini hayo yote yametokana na ushirikiano, mshikamano na kazi nzuri ambayo mliifanya na kuiwezesha TANAPA  kung'aa na mimi kama kiongozi wake niweze kutambuliwa na viongozi wa ngazi na kitaifa."


"Nina waomba endeleeni kuwa na mshikamano huo katika kufanya kazi zenu za kila siku huku, hekima na busara vikitawala pamoja na kuwepo kwa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya uhifadhi na utalii maana umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu."


Awali, akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella alimpongeza Dkt. Kijazi kwa kupata mafanikio makubwa katika utumishi wa umma, na mkoa wa Arusha unajivunia mchango mkubwa wa TANAPA katika kukuza pato la mkoa na kwa mtu mmoja mmoja.


"Nichukue fursa hii adhimu kukupongeza kwa mafanikio yako makubwa katika utumishi wa umma na sisi kama mkoa wa Arusha tunatambua mchango wako kupitia TANAPA ambao ni mdau mkubwa wa maendeleo nchini na hasa katika mkoa wetu kwa kuwa makao makuu yake yapo hapa."


Kaimu Kamishina wa Uhifadhi TANAPA Juma Kuja, alisema kuwa Shirika linathamini na litaenzi mazuri yote aliyoyafanya katika uongozi wake katika kuimarisha uhifadhi na kukuza utalii.


Hafla na tafrija makhususi ya kumtakia maisha mema baada ya utumishi uliotukuka wa Kamishna  wa Uhifadhi Mstaafu Dkt. Allan Kijazi ilifanyika jana jioni tarehe 16.11.2023 katika Ukumbi wa AIM Mall mtaa wa Majengo jijini Arusha.



Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa