Na Elinipa Lupembe
Kanisa Katholiki kupitia Kituo cha Malezi ya watoto cha St. Mary's Children's, limepongezwa kwa kutekeleza miradi ya maendeleo inayotoa huduma kwa jamii chini huku Serikali ikithamini mchango wa kanisa hilo.
Pongezi hizo zimetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu, Godfrey Eliakimu Mnzava, muda mfupi kabla ya kuweka Jiwe la Msingi kwenye Kituo hicho, kilichojengwa na Kanisa wenye thamani ya shilingi milioni 950, kilichopo kata ya Kikwe Halmashauri ya Meru wilaya ya Arumeru leo Julai 19, 2024.
Amesema kuwa, licha ya Kanisa hilo kutoa huduma za kiroho kwa karne kadhaa sasa lakini limekwenda mbele zaidi katika kutoa huduma kwa jamii katika seka za afya, elimu na kutekeleza miradi mingi kwa kuwa na Programa mbalimbali na endelevu za kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji na majitaji maalum.
Ndugu Mnzava kabla ya kuweka jiwe la Msingi, amepongeza ujenzi wa Kituo hicho cha Kulelea watoto wenye mahitaji Maaluku na kusisitiza kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wa kanisa hilo katika kutoa huduma kwa jamii ambazo kimsingi lilikuwa ni jukumunla Serikali.
"Serikali inathamini sana mchango mkubwa wa Kanisa Katholiki kwa jamii, hivyo ni vema wananchi tuendelee kutumia fursa zinazotolewa na kanisa kwa Maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla wake". Amesema Mnzava
Hata hivyo ametumia wasaa huo kutoa Jumbe za Kidumu za Mwenge wa Uhuru, ikiwemo mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malari, matumizi ya Dawa za Kulevya, VVU - UKIMWI sambamba na kuhamasisha wananchi kuzingatia Lishe Bora pamoja na kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kujiandikisha kwenye daftari la Wapiga kura.
Aidha amewahimiza wananchi kuepukana na Rushwa na kuacha tabia ya kuifanya Rushwa kuwa sehemu ya maisha yetu na kuwasisitiza kuichukia Rushwa na kuifanya ni adui wa haki na maisha ya bimadamu.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 ni "Tunza Mazingira, Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu"
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa