Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka ameiagiza Ofisi ya msajili wa hazina na Wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa Taasisi za umma kuendelea kuimarisha usimamizi wa taasisi zao ili kukuza ufanisi na utendaji wa taasisi hizo.
Balozi Kusiluka ametoa maagizo hayo leo Ijumaa Agosti 30, 2024 wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa wakuu hao wa Taasisi kwenye kituo cha kimataifa cha AICC jijini Arusha akielekeza pia kutekelezwa kikamilifu kwa maagizo na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati wa kufungua mkutano huo.
"Mmekuwa na section nzuri sana na kama alivyosema Msajili wa Hazina juzi wakati wa kufungua kuwa kwa wingi wenu na huu mchanganyiko hii ni thinkTank kubwa sana ya serikali labda hatuna mkusanyiko mkubwa namna hii ambayo serikali imewekeza kwenu. Mliyojadili na kuazimia kama serikali tutawasaidia kuona yanatekelezeka." Ameongeza Balozi Kusiluka.
Katika Mkutano huo wa siku tatu uliotamatika mapema leo mchana, jumla ya maazimio na makubaliano sita makubwa na madogo 17 yamefikiwa yakihusu taasisi na mashirika yote ya Umma nchini Tanzania.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa