Jumla ya wanafunzi 1,582,140 kufanya mtihani wa upimaji wa Kitaifa Darasa la IV Tanzania Bara kwa mwaka 2025.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa Barqza la Mitihani la Taifa (NECTA) Prof. Said Ali Mohamed, amesema watahiniwa hao 1,582,140 wamesajiliwa kufanya mtihani huo kwenye jumla ya shule 20, 517 ikiwa na onhezeko la shule 448 ikilinganishwa na mwaka 2024.
Idadi hiyo ya watahiniwa imejumiusha wavulana ni 764,290 sawa na 48% na wasichana 817,850 sawa na 52%
Awali ameweka wazi kuwa, mtihani huo utafanyika kwa siku mbili tarehe 22 na 23 Oktoba,2025.

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa