Mkuu wa Mkoa wa Arusha ameziagiza halmashauri zote za mkoa huu kutenga kiasi cha shilingi 1000 kwa kila mtoto katika halmashauri kutoka katika mapato ya ndani ilikusaidia katika mfuko wa Lishe wa halmashauri.
Yamesemwa hayo na katibu tawala wa Mkoa Richard Kwitega kwa niaba ya mkuu wa mkoa alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja ya namna ya upangaji wa bajeti ya lishe katika mkakati wa lishe Kitaifa, amesema hali ya udumavu katika mkoa si nzuri sana upo kwa asilimia 36.
Amesema wahanga wakubwa ni watoto na wanawake ambapo watoto wengi wanaudumavu wa akili na mwili na wanawake wajawazito hujifungua watoto njiti au hupoteza maisha kabisa.
Hali za watoto kwa mkoa wa Arusha kwa mwaka 2015/2016 watoto wenye uzito mdogo kwa urefu ni asilimia 6.5 na wenye uzito mdogo kwa umri ni asilimia 20.1 na watoto 57 kati ya 100 wana upungufu wa damu.
Amesema hali hii pia kwa akinamama wajawazito sio nzuri kwani wanawake wenye umri kati ya miaka 15 hadi 17, 14 kati ya 100 wana upungufu wa damu kwa takwimu za mwaka 2015/2016.
Akisisitiza zaida mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amesema ifike wakati sasa elimu itolewe kwa kina juu ya ulaji mzuri wa vyakula mbadala vitakavyo ongeza virutubisho mbalimbali katika mwili badala ya kutumia madawa kwa wingi.
Amesema vyakula kama mbogamboga, matunda na vyakula vya nafaka vinavyoongeza madini, vitamin na virutubisho vingine mbalimbali yanayoitajika mwilini.
Pia, mpango mkakati wa lishe unaitaji bajeti ambayo utasimamia utekelezaji wake kwa kiasi kikubwa, amesema mafunzo hayo waliyopatiwa yatawasaidia kuwa na uwelewa mpana wa namna ya kusimamia shughuli nzima za lishe katika wilaya zao kwa ufasa.
Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wa kutengeneza bajeti za lishe katika mkoa wa Arusha yaliyosimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) yalifanyika kwa kuhusisha wilaya mbili ya Jiji la Arusha na Arusha Vijiji na kuendelea katika wilaya nyingine za Meru, Longido,Monduli,Karatu na Ngorongoro.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa