WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Watu Wenye Ulemavu ,Ridhiwani Kikwete, amewaagiza Maofisa Kazi, kufanya kaguzi za mara kwa mara kwenye maeneo ya kazi, ikiwemo viwanda na migodi ili kubaini mapungufu yaliyopo na kuchua hatua stahiki.
Ridhiwani aliyasema hayo jana Jijini Arusha wakati wa akifungua Kikao Kazi cha Maofisa Kazi kutoka mikoa yote Tanzania Bara ,kilichoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na kuwataka Maofisa hao kukagua maeneo ya viwanda na migodi kwani kumekuwa na malalamiko ya ukosefu wa vifaa vya kazi huku wengine wakifanya kazi kwenye mazingira magumu.
Amekuwa akipokea malalamiko mengi ya wafanyakazi kutoka kwenye migodi wakikabiliwa na mazingira magumu ya kazi,hivyo kuwataka kuweka utaratibu wa kunywa maziwa baada ya kazi kutokana na mazingira halisi yaliyopo, malalamiko ambayo hayana majibu, nendeni mkafanye ukaguzi na kutatua kero hizo".Amesema
Alisema pia vibali vya kazi haswa baadhi ya maeneo hususan Mkoa wa Dar es Salaam kwani yapo malalamiko kuna watu wanaingizwa kinyemela bila kuwa na vibali vya kazi jambo hilo halikubaliki na wajue wanaikosesha serikali mapato lakini pia wanawanyima haki watanzania wenye sifa stahiki katika baadhi ya kazi
"Mfano kunabaadhi ya maeneo nafasi ya Ofisa Rasilimali Watu amejiriwa kutoka nje ya nchi na kazi ya HR ni kutambua watu anaofanya nao kazi sasa inakuwaje unakuwa na ofisa asiye mtanzania kwenye kazi ,hebu maofisa kazi timizeni makujumu yenu,nyie mwenzenu mimi hakuna mkubwa hapa zaidi ya Rais Samia Hassan Suluhu "
Alisema inashangaza kuona baadhi ya viwanda kwenye mikoa mbalimbali haswa Mkoa wa Dar es Salaam kunaofisa rasilimali watu (HR) amejiriwa kutoka nje ya nchi ,unajiuliza ameajiriwa kwa kigezo gani na kwanini asiajiriwe ofisa kutoka ndani ya nchi ambaye anajua mazingira husika ya nchi yake.
"Niambieni mazingira yenu mnayofanyia kazi kama kunachangamoto semeni hata mtu amepata kibali cha kazi na hukijui semeni ,najua kunavibali feki lakini mkivibaini semeni na nyie maofisa kazi mnawajibu huo na kila mwezi nipewe taarifa za hali za kazi ili tujue kunashida gani na kuzifanyia kazi kupitia mikoa yenu mnayosimamia"
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),Dk,John Mduma alisema mfuko huo unaendelea kulipa fidia kwa wafanyakazi,wategemezi lakini pia wanaendelea kujiimarisha kwa kutuma mitandao na sasa huduma wanazozitoa zipo kieletroniki ili kuhakikikisha wateja wanafurahia huduma bora.
Alisisitiza pia WCF inpokea maombi ya vibali vya kazi na mada mbalimbali zitatolewa kwa washiriki hao katika kuboresha utendaji kazi wa Mfuko huo
Wakati huo huo,Mkuu wa Huduma za Sheria kutoka WFC,Abraham Siyovelwa alisema urekebishwaji wa Sheria ya fidia kwa wafanyakazi utasaidia kulinda zaidi maslahi ya wanufaika ikiwemo kuweka mazingira bora ya kupata vigezo pia pale mfanyakazi akipata ajali akiwa kazini atalipwa fidia hadi mwisho wa maisha yake .
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa