Maeneo yatakayofanya uchaguzi tarehe 27 Novemba, 2024 kwa sasa ni vijiji 12,280 kutoka Vijiji 12,333 vilivyotangazwa hapo awali, mitaa 4,264 tofauti na mitaa 4,269 iliyotangazwa hapo awali na vitongoji 63,886 ukilinganisha na vitongiji 64,274 vilivyotangazwa kwenye gazeti la Serikali Tangazo Na.796 na 797 yote ya tarehe 06 Septemba, 2024.
Mabadiliko haya yemetokana na Halmashauri za Wilaya za Kaliua, Nsimbo na Tanganyika kuwa na makazi ya Wakimbizi ya Ulyankulu, Katumba na Mishamo, na wananchi kuhama kwenye baadhi ya vitongoji kutokana na sababu mbalimbali.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa alipokua akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mchakato wa kuchukua, kurejesha, uteuzi pamoja na rufaa za wagombea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa