• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

MAFANIKIO YA MKOA KWA MWAKA 2017

Posted on: December 29th, 2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 UTEKELEZAJI NA MAFANIKIO YA SHUGHULI ZA SERIKALI MKOA WA ARUSHA JANUARI HADI DISEMBA 2017

UTANGULIZI

Mkoa wa Arusha ni moja kati ya Mikoa 26 ya Tanzania Bara, wenye ukubwa wa Km za mraba 34,515.5. kiutawala Mkoa unao Wilaya sita Halmashauri 7, Tarafa 23, Kata 33, Vijiji 393, mitaa 154 na vitongoji 1471.

Idadi ya watu kwa ongezeko la 2.7% kwa mwaka inakadiriwa kufikia jumla ya watu wapato 1,835,787 wanawake wakiwa 51.5% na wanaume 48.5%.

UCHUMI 

Shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Arusha hasa hasa za kilimo na wafugaji ambao huchangia 20%, biashara huchangia 10.9%, viwanda na sekta nyingine huchangia 15.5%.

Pato la Mkoa limefikia Tsh. Trilion4,876, ambalo huchangia asilimia 4.77 kwenye pato la Taifa. Pato la Mkoa kwa mwaka ni (per capital income Tsh. 2,576.517).

HALI YA USALAMA

Hali ya ulinzi na usalama ya Mkoa ya Mkoa wa Arusha ni ya kuridhisha hasa baada ya juhudi kubwa kuwekwa na vyombo vya ulinzi na usalama kudhibiti mianya ya matuko yanayosababisha uvunjivu wa Amani. Wananchi wameendelea na shughuli za uzalishaji mali na kukuza kuhusu bila hofu yoyote ya usalama wao wa mali zao.

 

TAARIFA ZA SEKSHENI NA VITENGO

  • SEKSHENI YA UTAWALA NA RASILMALI WATU

MAFANIKIO

  • Imeweza kufanya Mafunzo kwa Maafisa Utumishi wote wa Halmashauri na Taasisi zipatazo 22 ambapo Maafisa 48 walipewa Mafunzo kwa undani kuhusu Sheria na taratibu za kuchukua kuhusu mashauri ya Kinidhamu, wamejifunza kuhusu kupima Utendaji kazi wa wazi OPRAS na wamejifunza kuandaa bajeti ya mishahara ambayo huko nyuma hawakuwahi kupata mafunzo hayo.
  • Seksheni imewezesha watumishi 39 kwenda masomoni kwa kada mbalimbali na hasa za afya kwa masomo ya muda mrefu.
  • Seksheni katika kusimama ustawi wa watumishi wake imetoa mafunzo na upimaji wa afya kwa watumishi wa RS na MSM wote kwa kupimwa magonjwa sugu yasiyoambukiza na virusi vya ukimwi jambo ambalo limefanyika kwa ufanisi.
  • Seksheni imeweza kuendesha mafunzo kwa Maafisa Utumishi ambapo mada ziliwasilishwa na Wataalamu toka Ofisi ya Rais Utumishi. Mafunzo haya yamekuwa dira kwa Maafisa Utumishi.
  • Seksheni imeweza kusimamia, na kuratibu, ziara mbalimbali za kikazi za viongozi, za ndani na nje ya Mkoa na hata nje ya Nchi, hasa za Mheshimwa Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa pamoja na viongozi na watendaji wengine.

 

  • SEKSHENI YA UCHUMI NA UZALISHAJI MALI

Sekta ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji

Mkoa wa Arusha ni moja ya Mikoa iliyopiga hatua kubwa katika maendeleo ya viwanda hapa nchini. Kuna Viwanda  Vikubwa 38, vya Kati 131 na Vidogo 2165 vinatoa ajira zaidi ya 50,000 na vinachangia asilimia 10.9 ya pato la Mkoa.

  • Kwa kipindi cha miaka miwili yaani 2016/2017 na 2017/2018 - Mkoa unajumla ya Viwanda 35 vipya vilivyo katika hatua mbalimbali ambavyo vinakadiriwa kutoa ajira kati ya 600 hadi 700. Aidha Mkoa kupitia Halmashauri zake umetenga maeneo ya ekari 77,110 kwa ajili ya Uwekezaji. Kati ya hizo ekari 4100 zimeanza kufanyiwa mpango wa kupimwa viwanja 171 kwa ajili ya viwanda na uwekezaji katika eneo la Malula halmashauri ya Wilaya ya Meru na Wasso Ngorongoro.
  •  
  • Sekta ya Kilimo
  • Ujenzi wa Ghala la Kuhifadhi Vitunguu Karatu.

Serikali kupitia Programu ya MIVARF imejenga ghala la kuhifadhi vitunguu kwa ajili wa wakulima wa zao hilo pamoja na miundombinu ya ya barabara katika Tarafa ya Eyasi, Wilaya ya Karatu. Mradi huo umegharimu jumla ya Shilingi za kitanzania 1,530,450,036/- ambayo asilimia 95 ni ya Mradi na asilimia 5 ni ya Halmashauri ya Wilaya ya Karatu uwezo wa kuhifadhi vitunguu hadi tani 2400.

Mradi huu tayari umekamilika na tayari wakulima wote wanaendelea kuhifadhi vitunguu na kuanzia tarehe 1/12/2017 shughuli zote za biashara ya vitunguu zimeanza kufanyikia ndani ya eneo la Ghala hilo kama soko pekee kwa ajili ya kuendeshea shughuli ya biashara ya vitunguu. 

Wakulima wameishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kondoa kero iliyodumu kwa muda mrefu ambapo kulikuwa na wavamizi kutoka Nchi jirani katika mashamba yao ambapo walikuwa wakinunua mazao yangalipo mashambani kwa bei waliyoamua wao.  Tangu kujengwa kwa mradi huo, bei ya vitunguu imeongezeka kutoka TSh. 40,000 Kwa gunia hadi Tsh 100,000 kwa gunia baada ya mradi, baada kuhifadhiwa katika ghala hilo na kuuzwa katika soko halali linaloendeshwa eneo hilo la ghala.

Pamoja na mafanikio Serikali imegundua bado kuna matumizi yasiyo sahihi ya vipimo hivyo inahitajika kutoa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo ili wakulima wasiendelee kupunjwa na Serikali kukosa mapato halali

 

Sekta ya Mifugo

Ujenzi wa Soko la kisasa la mifugo

Ujenzi wa Soko la kisasa la mifugo katika Kijiji cha Eworendeke Wilayani Longido ambalo lipo kwenye hatua za mwisho za ujenzi chini ya Programu ya MIVARF. Ujenzi huu umegharimu kiasi cha Tsh. 782,050,572 ambayo asilimia 95 ni ya Mradi na asilimia 5 ni ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido. Uwepo wa Soko hili utasaidia kupunguza kero ya utoroshwaji wa mifugo kwenda Nchi jirani, kuongeza uzalishaji wa Mifugo na mazao yake kutokana na uwepo wa uhakika wa soko la mifugo. Pia kuboresha na kuinua kipato cha wananchi kwa kuuza mifugo ndani ya Tanzania  na Nchi jirani, ajira kwa vijana na wanawake pamoja na kuipatia Serikali mapato ambayo yalipotea kwa muda mrefu kutokana na utoroshwaji wa mifugo  kwenda nchi jirani.

Aidha, uwepo wa soko hili utasaidia kuhifadhi mazingira yaliyokuwa yanaharibiwa na mifugo waliokuwa wakitoroshwa kwa kuswagwa kupitia njia zisizo rasmi kwenda Nchi jirani.

 

 

Sekta ya Maliasili Na Utalii Na Uhifadhi Wa Mazingira 

Kuondolewa malango ‘Gates’ ukanda wa ziwa Natroni

Sekta ya Utalii imekumbwa na changamoto ya muda mrefu wa uwepo wa Mageti katika ukanda wa Ziwa Natroni ambapo mageti yalikuwa yamewekwa kila mpaka wa Halmashauri za Wilaya ya Monduli, Longido na Ngorongoro. Mwaka 2017/2018 Mkoa kupitia Mhe. Mkuu wa Mkoa umefanya jitihada za Kuhakikisha keKuondolewa malango ‘Gates’ matatu ambayo yalikuwa kero kwa wageni “Tourists” mwelekeo wa ukanda wa Ziwa Natroni katika Halmashauri za Wilaya ya Monduli, Longido na Ngorongoro.  Baada ya jitihada mbalimbali yalifikia kubakisha lango moja linalokusanya mapato kwa ufanisi.

Kumekuwa na ongezeko la  wageni/watlii wanaotembelea vivutio (“Number of Visitor Arrivals”) ambapo mwaka 2016 watalii 1,284,279 na "projection" kwa mwaka 2017 ni 1,436,480 na inatarajiwa kuongezeka. Aidha, asilimia 80 ya Watalii wanaofika Tanzania hufika/kupita Mkoa wa Arusha.

Mapato yatokanayo na Utalii yamekuwa yakiongezeka kutoka trilioni 3.71 mwaka 2015 hadi trilioni 4.64  Mwaka 2016; Aidha, mapato yanakadiriwa kuongezeka kwa kulinganisha mapato ya mwezi Januari – Novemba, 2017 NCAA na TANAPA pekee, Jedwali Na. I: limeainisha takwimu za mapato kitaifa kwa mwaka 2015 & 2016 na mapato ya Januari - Desemba, 2017 ya NCAA na TANAPA. Mapato mengine ya Utalii yanatokana na Utalii wa Picha, Utalii wa Uwindaji na Utalii wa Utamaduni na (WMA).

Jedwali Na. I: Takwimu za mapato kitaifa kwa mwaka 2016 & 2017, pia mapato ya Mwezi Januari – Novemba, 2017 kwa upande wa NCAA na TANAPA.


MWAKA

MAPATO KITAIFA

TANAPA

NCAA

2016        
Trilioni 4.64

-

-

Januari-Novemba, 2017

-

138.7bilioni

-

Januari -  , 2017

-

-

65.6bilioni
2015 - 2016
Ongezeko;
Bilioni 87

-

-


Chanzo: Kitabu cha Takwimu za Utalii cha Wizara ya Maliasili na Utalii, Idara ya Utalii, Mwaka 2016 ; NCAA & TANAPA, 2017

Mradi wa Kukabilinana na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Kwa muda wa zaidi ya Mikaka 10 Mkoa wa Arusha umekwa ukikabilia na mtawanyiko hafifi ambao umesababisha upungufu wa maji,  malisho na na hata kusababisha mifugo kufa na upungufu wa uzlishaji wa mazo ya chakula na biashara. Serikali kwa kushikiana na Mashirika yasiyo ya Kiserikali IIED na Hakikazi Catalyst wametekeleza kwa kasi Miradi 34 ambayo inagharimu Tsh. 1,908,015,342 kwa ajili ya kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi katika Halmashauri Za Wilaya za Longido, Monduli na Ngorongoro.

 

Baraza la Uwezeshaji

Mafanikio ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Katika Mkoa Wa Arusha Mwaka wa Fedha 2016/2017.

Makundi ya Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu ni muhimu katika ujenzi wa Taifa letu hususan katika Nyanja ya uchumi. Ili kufikia uchumi wa kati unaotegemea tasnia ya viwanda Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kuongeza makusanyo ya ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hali iliyopelekea ongezeko kubwa la idadi ya Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu kunufaika mikopo ya 10% inayotengwa kwenye makusanyo ya ndani. Aidha, uwezeshaji kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu katika mwaka wa fedha 2016/2017 kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa ni jumla ya Tshs. 2,554,500,000/= kwa vikundi 279 vya vijana na vikundi 370 vya wanawake. Ambapo vijana Tshs. 1,059,000,000/= na wanawake Tshs. 1,495,500,000/= ikiwaazma kubwa ni kuongeza ushiriki wa shughuli za kiuchumi na uzalishaji mali katika makundi haya muhimu ya ujenzi wa Taifa.

Mkoa unaendelea kumuunga mkono Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, juhudi za kuongeza ushiriki wa wanawake katika shughuli za kiuchumi na uzalishaji mali kwa kuzindua Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi. Aidha, majukwaa 116 yamezinduliwa katika ngazi ya Mkoa, Wilaya na Kata, ambapo jukwaa 1 la Mkoa, majukwaa 7 ya Halmashauri na majukwaa 108 yaKata kati ya Kata 158 yakiwa na lengo kuu la kuelimisha nguzo tisa za Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004. Hali iliyopelekea Mkoa kupata tuzo ya Taifa ya uwezeshaji, kwa kushika nafasi ya kwanza kati ya Mikoa 26 ya Tanzania Bara katika mwaka wa fedha 2016/2017.

Sekta ya Ushirika

Vyama vya Ushirika 12 vya walaji (Consumers) vimeandikishwa katika Tarafa ya Ngorongoro. Lengo ni kusaidia wananchi kuapata bidha/chakula kwa urahisi na bei nafuu ili kuweza kukabilina na hali ya ukame.

  • SEHEMU YA MAJI

Jitihada za kuondoa kero ya upatikanaji MAJI:

Maji vijijini.

  • Hadi kufikia Desemba 2016 Hali ya utekelezaji wa miradi ya vijiji 10 katika halmashauri (Programu ya Maji Vijijini) ilikuwa ya kusuasua kutokana na Wakandarasi wengi kusitisha utekelezaji wa kazi za miradi hiyo kutokana na madeni makubwa waliyokuwa wanadai.
  • Hali ilivyo sasa Serikali imelipa madeni ya Wakandarasi hao kufikia kiasi cha Bilioni 2.651na inaendelea kulipa Wakandarasi wanaohusika kulingana na kadri kazi zinavyofanyika. Aidha usimamizi kwa sehemu kubwa ya kazi hizo kwa sasa unafanyika na wataalamu wa Halmashauri kwa kushirikiana na Mkoa baada ya wataalamu washauri kujitoa kutokana na madeni waliyokuwa wanadai. Hali ya utekelezaji kwasasa imeongezeka ambapo miradi kumi zaidi imekamilika kutoka 19 mwaka jana hadi kufikia 29 sasa, hivyo watu 143,572 wameanza kupata maji baada ya kusubiri muda mrefu toka miradi hiyo ianze.
  • Kwa msukumo huu wa Serikali tunatarajia hadi kufikia Juni 2018 miradi 33 zaidi itakuwa imekamilika na watu takribani 450,000 wataanza kupata huduma ya maji, hali hii itanyanyua upatikanaji wa maji  vijijini kutoka asilimia 58.6 sasa hadi kufikia asilimia 65.
  • Mradi wa vijiji vitano unaochangiwa na Serikali kwa Bilioni 1.3 na DFID kwa Bilioni 4.5 umeanza katika halmashauri ya Arusha ambapo tunataraji watu 50,000 zaidi wataanza kupata huduma ya maji hadi kufikia Desemba 2018.
  • Huu ni mwendelezo wa kuelekea kwenye lengo la Serikali la kutoa huduma ya maji kwa 85% vijijini ifikapo 2020.
  • Maji Mjini
  •  
  • Maji kwa jiji la Arusha :
  •  
  • Kuanza kwa mradi mkubwa wa 476 bilioni( chini ya AUWSA mkopo nafuu kutoka AfDB) :
  • Hatua ya Upembuzi yakinifu imekamilika na sasa utekelezaji wa miradi ya kuongeza upatikanaji maji kwa jiji la Arusha kutoka 42.9% hivi sasa hadi kufikia 100%miaka 2 ijayo umeanza na uchimbaji wa visima virefu 11 katika shamba la Mbegu (ASA) umeanza na unaendelea mradi huu ulizinduliwa na Mhe. Waziri wa Maji na Umwagiliaji mwezi Oktoba, 2017; mradi pia unalenga kuinua huduma ya uondoaji majitaka katika jiji kutoka 7.6% hivi sasa hadi kufikia 30% utakapokamilika.
  • Maji kwa Mji wa Longido ( Utekelezaji chini ya AUWSA kwa niaba ya Serikali):
  •  
  • Mradi wa kupeleka majisafi katika mji wa Longido kwa kutokea mto simba uliopo katika wilaya ya Hai – Kilimanjaro takribani km.69 umeanza na unaendelea kujengwa, kiasi cha 16 bilioni zitatumika na mradi utaondoa tatizo la huduma ya maji kwa mji huu ambao kwa sasa huduma ya maji ni chini ya 20% hadi kufikia zaidi ya 85% hii ni pamoja na vijiji vya Orbomba, Ranchi na Engikareti; kwa sasa utekelezaji umefikia zaidi ya 50% na inategemewa ifikapo Juni, 2018 mradi utakuwa umekamilika. Mradi ulizinduliwa na Mhe. Waziri Mkuu mwezi, Septemba, 2017.

Usimamizi wa Huduma za maji katika makao makuu ya wilaya:

  • Kwa sasa Miji mikuu yote yawilaya (6)ina bodi za usamamizi wa Mamlaka zao za maji ukilinganisha na Bodi tano 5 zilizokuwepo kufikia Desemba 2016. Aidha pia imeongezeka Bodi ya usimamizi wa Mamlaka ya maji ya Mji mdogo wa Ngaramtoni.
  • Wastani wa upatikanaji maji mijini mpaka sasa kimkoa ni 42.9% na lengo ni kufikia 95% kwa miji mikuu ya mkoa na 90% kwa miji ya wilaya ifikapo 2020 kama inavyoelekezwa na Serikali.
  • Utekelezaji wa miradi 2 tajwa hapo juu utainua wastani wa upatikanaji wa huduma ya maji mijini hadi kufikia 80% ya mahitaji.
  • Kusogeza huduma za maji kwa wananchi wenye adha kubwa ya huduma ya maji kupitia Mamlaka za Maji :
  •  
  • Mamlaka za Maji kwa kiasi kikubwa zimejenga uwezo mkubwa katika kutoa na kuendeleza huduma za maji  hata nje ya mipaka yake na kusogeza huduma kwa wananchi wenye uhitaji mkubwa au wanaokabiliwa na adha kubwa ya maji  kama ifuatavyo:
  • AUWSA wamesogeza huduma kwa wananchi wa vijiji vya Halmashauri ya Arusha – maeneo ya Burka, Kisongo na Matevesi.
  • Mamlaka ya maji Monduli kupitia chanzo chake cha maji inapeleke maji kwa vijiji vya Meserani Juu na sasa kuna mradi unaendelea kupeleka maji kwa wananchi wa Lendikinya na hapo baadaye Mtimmoja na Nanja .
  • KITENGO CHA SERIKALI ZA MITAA
  • Kwa Mwaka 2016/17 Halmashauri za Mkoa wa Arusha zilikusanya julma ya shilingi 27,347,677,414 ikiwa ni asilimia 95% ya makisio 28,909,733,983 waliokuwa wamepanga.Makusanyo hayo yameongezeka kwa asilimia 19 yakilinganishwa na makusanyo ya mwaka 2015/16 ambayo yalikuwa 22,731,853,820 sawa na asilimia 76 ya makisio ya 29,883,651,008 yaliyokuwa yamepangwa. Ongezeko hili la makusanyo ya ndani ya Halmashauri ni matokeo ya usimamizi mzuri, matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa makusanyo ya mapato ya ndani (Local Government Revenue Collection Information System – LGRCIS) unaotumika katika Halmashauri zote na matumizi ya Points of Sales (POS) katika kila chanzo. Jedwali lifuatalo linaonesha makusanyo kwa kila Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2016/17.


HALMASHAURI

MAKISIO

MAKUSANYO

ASILIMIA

ARUSHA CC

12,299,585,000

13,603,884,903

111%

ARUSHA DC

3,200,600,000

2,944,941,862

92%

MERU DC

3,627,024,000

3,411,094,173

94%

LONGIDO DC

1,343,549,980

   904,070,011.17

67%

KARATU DC

3,887,383,000

2,731,081,486

70%

NGORONGORO DC

2,094,282,000

1,542,484,157

74%

MONDULI DC

2,415,317,000

2,210,120,822

90%

JUMLA

28,909,733,983

27,347,677,414

95%


  • Kwa mwaka wa fedha 2017/18 Halmashauri za Mkoa wa Arusha zimekasimia kukusanya jumla ya shilingi 31,642,381,000 kutoka kwenye vyanzo vya ndani. Hadi kufikia tarehe 30 Novemba, 2017 jumla ya shilingi 12,178,915,825 sawa na asilimia 38.49 zilikuwa zimekusanywa. Jedwali lifuatalo linaonesha makusanyo kwa kila Halmashauri hadi kufikia tarehe 30 Novemba, 2017


HALMASHAURI

MAKISIO

MAKUSANYO

ASILIMIA

ARUSHA CC

14,580,000,000.00

5,976,702,539.00

40.99

ARUSHA DC

3,493,318,000.00

1,304,011,053.00

37.33

MERU DC

3,710,623,000.00

1,465,110,295.00

39.48

LONGIDO DC

1,039,747,000.00

519,552,217.00

49.97

KARATU DC

  2,211,206,000.00

   906,180,470.00

40.98

NGORONGORO DC

  4,177,604,000.00

1,268,922,171.00

30.37

MONDULI DC

  2,429,883,000.00

   738,437,080.00

30.39

JUMLA

 31,642,381,000

12,178,915,825

38.49


  • Mkoa umezisimamia na kuzijengea uwezo Kamati za ukaguzi za Halmashauri na mafanikio yameonekana katika ukaguzi wa Hesabu za Serikali ambapo Halmashauri Tano zilipata Hati Inayoridhisha za Ukaguzi ukilinganisha na mwaka uliopita ambapo ni Halmashauri tatu tu zilipata hati inayoridhisha.

HALMASHAURI

MWAKA 2014/15

MWAKA 2015/2016

ARUSHA CC

Hati inayoridhisha

Hati inayoridhisha

ARUSHA DC

Hati inayoridhisha

Hati inayoridhisha

KARATU DC

Hati isiyoridhisha

Hati yenye mashaka

LONGIDO DC

Hati yenye mashaka

Hati yenye mashaka

MONDULI DC

Hati inayoridhisha

Hati inayoridhisha

MERU DC
Hati yenye mashaka

Hati inayoridhisha

NGORONGORO DC

Hati yenye mashaka

Hati inayoridhisaha

  • Hadi kufikia Decemba 2017 Mkoa ulifanikiwa kutoa mafunzo kwenye Nyanja mbalimbali kama vile Utumishi, Fedha na Uchumi kwa Watumishi wa Halmashauri. Mafunzo haya yameboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa Wananchi ukilinganisha na Desemba 2016 ambapo Watendaji wa Halmashauri walikuwa hawajapata mafunzo husika.
  • Halmashauri zote kwa sasa zinatumia mifumo ya Kieletroniki katika kukusanya na kufanya matumizi ya fedha ukinganisha na Miaka iliyopita ambapo Halmashauri zilikuwa zinakusanya kwa kutumia mifumo lakini Matumizi yakifanyika kwa njia ya hundi. Utumiaji wa mifumo umeongeza udhibiti wa mapato na Matumizi.
  • SEKSHENI YA MIPANGO NA URATIBU

SEKRETARIET YA MKOA

1.Ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote 7 umefanyika, na jumla ya miradi 398 kati ya miradi 613 iliweza kukaguliwa kwa kipindi cha Julai hadi Juni 2016/2017.

Seksheni pia imeweza kukagua miradi 125 ya mwaka wa fedha 2017/2018 na mingi ya miradi hii ipo katika sekta za Afya, Elimu, Maji na Barabara.  Utekelezaji wa miradi hii upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na baadhi ya miradi imekamilika ikiwemo miradi ya ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu (6 in one), mabweni ya wanafunzi, ujenzi wa vituo vya afya, Zahanati na baadhi ya miradi ya Maji Vijijini

 

2. Uanzishwaji wa jukwaa la wanawake la Mkoa wa Arusha limeanzishwa na sasa wanawake wa mkoa wa Arusha wanazo fursa mbalimbali za kutumia jukwaa hili katika kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha biashara mbalimbali na kupata fursa ya kuunganishwa katika mtandao wa taasisi za kifedha zitakazoweza kuwakopesha kwa riba nafuu sana

3. Kwa upande wa programu ya TASAF III na OPEC III mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na

-  Mpango wa kunusuru kaya maskini ambapo katika Mkoa wa Arusha Jumla ya Kaya maskini 62,492 zikiwa na wanaume 5,059 na wanawake 41,771 zimeweza kutambuliwa baada ya kukidhi viegezo.

-  Jumla ya fedha Tshs 22,652,188,870.37 zilipokelewa katika Mkoa wa Arusha toka TASAF Makao Makuu kwa ajili ya malipo ya Kaya maskini zipatazo 46,771 katika Vijiji na Mitaa 290 tangu awamu ya kwanza  ya mpango huu Julai hadi Agasti 2015

-  Mkoa umefanikiwa kutekeleza miradi 63 ya ujenzi wa miundombinu mbalimabali ya Jamii, ikiwemo miradi ya sekta ya elimu, Afya, Barabara, mifereji ya umwagiliaji na mazingira, yenye thamani ya Tshas 2,748,468,978.39 (miradi 9 kwa kila Halmashauri ya Wilaya)

  • SEKSHENI YA ELIMU 

Uandikishaji wa wanafunzi wa kuanza Elimu ya awali na darasa la kwanza hadi Desemba 2016 ulikuwa wanafunzi 88,268 lakini hadi kufikia Desemba 2017, hali ya maoteo ya uandikishaji wa elimu ya Awali ni wanafunzi 102,411 (wav 52,142 was 50,269).

Mkoa umekuwa na ongezeko la madarasa ya Elimu ya Awali kutoka 647 Desemba 2016, hadi kufikia 715 Desemba, 2017 sawa na ongezeko la  9.23% shule  za msingi 690  Desemba, 2016 hadi shukle za msingi 723 Desemba, 2017 sawa na ongezeko la 4.56%  sekondari 230 Desemba, 2016 hadi shule 213 Desemba 2017 sawa na ongezeko la 0.43%.

Uchaguzi wa wanafunzi wa kuanza kidato cha kwanza hadi kufikia mwezi Desemba, 2016 ulikuwa ni wanafunzi 26,984(wav 12,583 was 14,401) sawa na 100% ya wanafunzi wote waliofaulu. Uchaguzi wa wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza Januari, 2017 ni 29,624(wav 14,215, was 15,409) ongezeko la wanafunzi 2,640. Wanafunzi wote waliofaulu sawa na100% wamepata nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza 2018.

Hadi Desemba, 2016 Mkoa ulikuwa na jumla ya shule 118 ambazo zilikuwa hazijasajiliwa na zilikuwa zinaendeshwa kinyume cha sheria ya Elimu Na. 24 ya mwaka 1978 na marekebisho yake ya 1995 na 2002. Lakini hadi kufikia Desemba, 2017 shule zote (BUBU) zisizo na usajili zimefungwa na wanafunzi wamehamishiwa kwenye shule zenye usajili.

Hadi kufikia Desemba, 2016 Mkoa kupitia Halmashauri zake haukuwa na mradi wowote chini mpango wa Lipa kwa Matokeo (P4R) lakini katika kipindi cha mwaka mmoja hadi Desemba 2017 Mkoa ulipokea Tsh. 1,036,000,000/= kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya shule mpya za kidato cha Tano za Mwandeti, Mlangarini, Nainokanoka na Loliondo na  kila shule ilipewa Tsh. 259,000,000/= za ujenzi  wa madarasa, maabara, bweni moja na matundu ya vyoo umekamika 100%. Ujenzi  bweni la pili umekamilika kwa 20%.

Mdondoko wa wanafunzi (Drop out) wa shule za msingi umepungua kutoka 18%  Desemba 2016 hadi kufikia 16% Desemba 2017 kwa wanafunzi walioanza darasa la kwanza ikilinganishwa na waliomaliza  darasa la Saba 2017. Lengo ni kuhakikisha mdondoko unapungua chini ya 10% mwaka 2018 na hatimaye kumalizika kabisa.

Kupitia Mpango wa Elimu bila Malipo, shule za msingi na Sekondari zimeendelea kupokea wastani wa Tsh. 1,842,990,926/= kwa mwezi ikiwa ni ruzuku ya uendeshaji wa shule ambapo shule za msingi zinapokea Tsh. 620,091,380/= na shule za sekondari zinapokea Tsh. 1,222,899, 546/=.

Hadi kufikia Desemba 2017 serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari na msingi maalum kwa watoto wenye mahitaji maalum. Gharama ya mradi huo ni Tsh. 4.5 bilion na awamu ya kwanza zimepokelewa Tsh. 1.2 bilioni na ujenzi unaendelea. Lengo ni kuhakikisha ujenzi umekamilika 2018.

Desemba 2016 vijana 200 waendesha pikipiki (bodaboda) walipewa mkoa wa pikipiki 200 usio na riba zenye thamani ya Tsh. 400,000,000/=. Kufikia tarehe 27 Desemba, 2017 kiasi cha Tsh. 284,851,644/= kimekwisha rejeshwa sawa na66.7% ya marejesho yote ambayo ni Tsh. 427,140,000/=. Wastani wa vijana waliorejesha ni 133.4 kati ya vijana 200 na wastani wa vijana ambao hawajarejesha ni 66.6 tu sawa na 33.3% kati ya vijana 200. Baada ya kukamilisha marejesho yote Tsh. 200,000,000/= zitabaki kama mtaji kwa vijana hawa na Tsh.200,000,000/= matarajio ya fedha zilizobaki kwa mwaka 2018 ni kuzielekeza kwa akina mama wamachinga kama mkopo ya mitaji isiyokuwa na riba.

 

  • SEKTA YA ARDHI

Katika sekta ya miundombinu mambo muhimumatano (5) yaliyoshughulikiwa ni pamoja na:-

  • Utatuzi wa mgogoro wa  Pori Tengefu la Loliondo, mgogoro ulioanza mwaka 1992, mgogoro  uliodumu kwa takribani miaka 25  na chanzo kikubwa cha mgogoro ni mgongano wa matumizi ya Ardhi unaotambuliwa na sheria mbili tofauti zinazotumika katika eneo moja yaani ni sheria ya Hifadhi ya Wanyama Pori Na. 5 ya mwaka 2009 na sheria ya Ardhi ya vijiji ya mwaka 1999.

Hivi sasa serikali imeshatolea maelekezo ya namna ya  utatuzi ikiwa ni pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kuandaa Muswada wa sheria utakowasilishwa serikalini kupitia Baraza la Mawaziri kuhusu sheria  Mahsusi ya eneo la Loliondo.

  • Utatuzi wa migogoro mbali mbali ya Ardhi
  • Mkoa umeshughulikia migogoro ya Ardhi iliyodumu kwa muda mrefu  124 kwa mwaka 2017 kutoka migogoro 42  iliyoshughulikiwa  mwaka 2016 sawa na ongezeko  la asilimia 192.2 na lengo ni kuhakikisha migogoro yote inatakyojitokeza mwaka 2018 itatatuliwa kwa wakati.

Aidha katika kutatua migogoro ya ardhi katika Jiji la Arusha jumla ya viwanja 163 vimetolewa kwa wananchi waliokuwa wanadai fidia ya viwanja mbadala katika eneo la Oljoro.

  • Kutenga maeneo ya uwekezaji na viwanda

Mkoa kupita Wilaya zake umehimiza kutenga maeneo ya uwekezaji na viwanda na bandari kavu ambapo mpaka hivi sasa jumla ya ekari 215,488.8 zimetengwa kutoka ekari 111,203 mwaka 2016 sawa na ongezeko asilimia 93.7.

Aidha malengo kwa mwaka 2018 ni kuhakikisha maeneo hayo yanawekewa miundombinu na kuhamasisha wawekezaji   na kuendelea kutenga maeneo mapya. Maeneo yaliyotengwa kwa kila Halmashauri ni kama ifuatavyo:-

  • Halmashauri ya Jiji la Arusha ekari 35.4
  • Halmashauri ya Wilaya ya Meru ekari 4,000
  • Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ekari 125,603.4,
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu 13,888.8
  • Halmashauri ya Wilaya ya Longido ekari 37.5
  • Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ekari 130.7 na
  • Halmashauri ya Wialya ya Monduli ekari 71,793
  •                                  Jumla 215,488.8
  • Kukamilika kwa Mpango Kambambe wa Jiji la Arusha na viunga vyake (Arusha Master Plan) ambapo hivi sasa umewasilishwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  kwa ajili ya kuidhimishwa, Jiji la Arusha lilikuwa na mpango kabambe ambao  uliisha muda wake toka mwaka 2016.

Upimaji wa maeneo ya  Taasisi za Umma, umeongozeka kutoka maeneo 62 mwaka  2016  hadi 134 mwaka 2017 ongezeko  lamaeneo 72  sawa na asilimia 116.

 

 

 

(B) SEKTA YA BARABARA

  • Mradi wa Ujenzi wa Barabara kutoka njia mbili hadi njia nne kutoka Sakina hadi Tengeru (14.1km).
  • Mradi wa ujenzi wa barabara ya mchepuko wa kusini (By Pass km. 42.41. kwa kiwango cha lami  barabara  ambayo haikuwepo  kwa gharama  Tshs.166,.016,742,402.
  • Mradi wa ujenzi wa barabara ya Mto wa Mbu – Loliondo
  • (Wasso – Sale Km 49).  Kwa kiwango cha lami Wilaya pekee katika Mkoa wa Arusha ambayo haikuwahi kuwa na lami. Mradi umeanza tarehe 18 Oktoba, 2017 na utagharimu Tshs. Billioni 87. Na utachukuwa jumla ya miezi 24 mpaka ukamilike.
  • Mradi wa ujenzi wa barabara ya KIA – Mererani kwa kiwango cha lami  Km.26 kutoka changarawe umekamilika.  Gharama za mradi zilikuwa ni Tshs. Bilioni 32.
  • Kijenge – Usa River (Nelsoni Mandela) Ujenzi wa Km.2 kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Tshs.Bilioni 1.48 uko mbioni kuanza.
  • Ongezeko  la Ujenzi wa mtandao wa  barabara za Jiji la Arusha kutoka Km.3.10  2016 hadi  Km 10.88 mwaka  2017  kwa fedha za msaada wa World Bank.
  • SEKTA YA AFYA MWAKA 2017

MAFANIKIO USAFI WA MAZINGIRA  

Kwa mwaka 2017 Mashindano yalifanyika kote nchini kwa kushirikisha ngazi ya Halmashauri za Wilaya,Manispaa, miji, Majiji, vijiji,Hospitali za Rufaa za Serikali na za binafsi pamoja na Hotel zenye hadhi ya nyota tano.

Mkoa ulifanya vizuri na kushinda tuzo zifuatazo:-

  • Katika Ngazi ya Halmashauri za Wilaya, Halmashauri ya Meru ilishinda nafasi ya kwanza na kuzawadiwa gari mpya aina ya Nissan Patrol
  • Ngazi ya Halmashauri za manispaa na majiji, Jiji la Arusha ilishinda nafasi ya pili nakuzawadiwa cheti na pikipiki 2 aina ya Yamaha
  • Ngazi ya Hoteli za kitalii, Hoteli ya Mount Meru ilishinda nafasi ya pili nakuzawadiwacheti .
  • Ngazi ya Hospitali za Rufaa za binafsi na za Serikali za Mikoa-
  • ALMC- nafasi ya kwanza- zawadi ya cheti cha ushindi nafasi ya kwanza
  • Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru mshindi wa tatu- zawadi ya cheti cha ushindi nafasi ya tatu
  • Ngazi ya Vijiji bora ni Kijiji cha Nambala- Meru DC- nafasi ya pili kitaifa – zawadi ya pikipiki mpya aina ya Yamaha.
  • Tupo kwenye mchakato wa kuendeleza dhana ya ushindi kwa kupanga mikakati ya kudumu kuendelea kuwa washindi.

USHIRIKI WA SEKTA BINAFSI NA ZA SERIKALI (PPP) 

Mkoaunatambua mchango mkubwa wa Wadau katika kuboresha huduma za Afya katika Halmashauri zetu na kukabiliana na majanga mbalimbali.

Katika mwaka wa fedha wa 2016/17 Mkoa kwa kushirikiana na Mdau wa Afya Leopard Tours and Safaris’ waliweza kukarabati jengo la kupimia wingi wa Virusi vya UKIMWI (Viral Load)katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ambalo limeshaanza kutoa huduma hivyo na kupelekea wagonjwa wanaotumia dawa kujua matokeo mapema na kupunguza gharama za usafirishaji wa sampuli kwenda KCMC. Mkoa pia unapokea sampuli kutoka Mikoa jirani ya Manyara na Singida. Hadi kufikia Desemba, 2017  idadi ya wagonjwa wa UKIMWI waliopimwa kwa kutumia vipimo vya Viral Load.

Uibuaji wa wagonjwa wa Kifua Kikuu

Kupitia ufadhili wa NTLP,Mkoa umeweza kuchagua  Maduka ya dawa binafsi na kuyajengea uwezo wa kutambua dalili za mwanzo za kifua kikuu ili kuwapa rufaa  kwenda kwenye maabara binafsi zilizoteuliwa kupima makohozi kwa lengo la  kuongeza kasi ya kuibua wagonjwa wa Kifua kikuu mapema. Jumla ya maduka 13 na maabara 5 zinatoa huduma hiyo.

Kupitia ufadhili wa KNCV,Mkoa umefanikiwa kuongeza uibuaji wa wagonjwa wa kifua kikuu mfano wamefanikiwa kuweka darubini ya kisasa (LED-Fluorence Microscopy) katika Halmashauri ya Longido na kupekelea kuongeza idadi ya wagonjwa kutoka 14 mpaka 61.Pia wameweka machine ya kisasa yenye uwezo wa kugundua vimelea vya kifua kikuu na usugu wa dawa za kifua kikuu (GXP-GeneXpert) amabayo imeweza kuibua wagonjwa wengi zaidi.

HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO

A: Ukarabati wa vyumba vya cPAC

  • Katika kupambana na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, kwa kushirikiana na wadau Engenderhealth wamesaidia kukarabati vituo 16 kati ya vituo 52 vinavyotoa huduma baada ya mimba kuharibika.
  • Ujenzi wa vyumba vya upasuaji 3 katika vituo vya kutoa huduma za Afya vimekamilika na kuanza kazi.

UUNDWAJI WA TIMU YA URATIBU WA AFYA MOJA “ONE HEALTH COORDINATION TEAM”

Mkoa wa Arusha umefanikiwa kuanzia Timu ya Afya moja (One health coordination team)  inayoshirikisha sekta mbalimbali katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali mfano magonjwa yanayoweza kuenezwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kama kimeta, magonjwa yanayohusisha maji kama kipindupindu na majanga mengine yanayosababisha madhara kwa afya ya binadamu. Tumefanikiwa kuelimisha jamii kuhusiana na magonjwa ya mifugo yanayoenezwa kwa binadamu, kuchukua sampuli 27 za binadamu kwa uchunguzi wa maabara wa kimeta ambapo 7 zilithibitishwa. Pia Mkoa umefanikiwa kutoa chanjo kwa mifugo 405,462(7%) kati ya mifugo 5,760,329.

UTOAJI WA TAARIFA YA MAGONJWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

Mkoa wetu umefanikiwa kutuma ripoti kwa ukamilifu kwa wastani wa asilimia 94 na kwa wakati asilimia 75  kwa mwaka 2017.

 

TAARIFA YA MAFANIKIO YA TAKWIMU (MTUHA)

Tumefanikiwa kushika nafasi ya nne ngazi ya Kitaifa katika uingizaji wa takwimu kwa wakati na usahihi (Jan-Jun 2017)

Mkoa umefanikiwa kushika nafasi ya kwanza  kitaifa katika utoaji wa taarifa za mwenendo wa kulaza wagonjwa (Bed Occupancy) kwa wakati na usahihi kwa mwaka  2017

 

MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA HOSPITALI YA MOUNT MERU

Ununuzi wa mashine ya kisasa ‘’Ultra-Modern Ultra sound with Dopler’’

Mkoa kwa kushirikiana na Mdau wa Afya kutoka Netherland wameweza kuinunulia Hospitaliya Mkoa ya Mount Meru ‘’Ultra-Modern Ultra sound with Dopler’’ yenye thamani ya Tsh.40,000,000/= ambapo inapima vipimo vifuatavyo:- 

Magonjwa na mapungufu mbalimbali ya mishipa ya damu  (Deep Venous thrombosis)

Kusinyaa kwa mishipa ya damu (Atherosclerosis)

Upimaji wa matiti (Uvimbe na saratani)

Kupima viungo vyote vya ndani ya mwili

Kupima hali ya ubongo kwa watoto baada ya kuzaliwa.

Kutokana na mashine hii, Hospitali yetu imeweza kupunguza kutuma wagonjwa nje kutafuta vipimo hivyo na kuongeza idadi ya wagonjwa wanaohitaji vipimo hivi kutoka nje ya Hospitali.  Vile vile tumeweza kuongeza mapato kutoka shilingi 1,228,587,852/= (2015/16) hadi 1,776,564,311 (2016/17) sawa na ongezeko la 45%.

  • KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI (RS)

Mambo Matano ya ufanisi katika Kitengo Cha Ukaguzi wa Ndani – Sekretarieti ya Mkoa wa Arusha ni yafuatayo;

  • Kitengo kimeweza kufanya ukaguzi katika kipindi hicho na kufanikiwa kutoa taarifa za kila robo mwaka kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Maelekezo mbalimbali ya Serikali. Hali hiyo imeimarisha usimamizi wa rasili mali za umma na utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika sekretarieti ya Mkoa wa Arusha. Taarifa hizo ni zifuatazo:
  • Taarifa ya Ukaguzi kwa robo ya Kwanza 2016/2017 (Julai-Septemba, 2016)
  • Taarifa ya Ukaguzi kwa robo ya Pili 2016/2017 (Oktoba-Desemba,2016)
  • Taarifa ya Ukaguzi kwa robo ya Tatu 2016/2017 (Januari-Machi. 2017)
  • Taarifa ya Ukaguzi kwa robo ya Nne 2016/2017 (Aprili-Juni, 2017)
  • Taarifa ya Ukaguzi kwa robo ya kwanza 2017/2018 (Julai-Septemba, 2017)
  • Kitengo kimeweza kuhakiki Madai mbalimbali ya Watumishi, Wakandarasi, wazabuni na Watoa huduma ambayo kwa kiwango kikubwa yalikubalika na kulipwa kwa kiasi kikubwa pia.
  • Kitengo kimeweza kushiriki kikamilifu zoezi la upitiaji na uchambuzi wa majibu ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za mwaka 2015/2016 kwa Halmashauri zote saba za Mkoa wa Arusha, na Ushauri ulitolewa ipasavyo.
  • Kitengo kimeweza kushiriki kikamilifu katika zoezi la upimaji wa awali ‘Mock Assessment’. Zoezi ambalo linazipima Halmashauri kuona kama zimefanya maandalizi kwa ajili ya kukidhi vigezo vya kupatiwa fedha za ruzuku ya maendeleo (LGDG)
  • KITENGO CHA TEHAMA

Mafanikio katika mwaka 2017 kitengo cha TEHAMA.

  • Kusimika Mfumo wa Uendeshaji na Usimamizi  wa Vituo vya Kutolea huduma za Afya (GoT- HoMIS) katika Hospitali ya Mkoa na za wilaya za Mkoa wa Arusha, ambazo ni;
  • Hospitali ya Wilaya ya Arusha (Oltrument).
  • Hospitali ya Wilaya ya Meru, 
  • Hospitali ya Wilaya ya Monduli
  • Kituo cha Afya Karatu.
  • Kituo cha Afya Waso (Ngorongoro Dc)
  • Kituo cha Afya daraja mbili (jiji)

Kwa upande wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na vituo vya afya mapato yameongezeka kwa marambili zaidi ukilinganisha na kipindi cha awali kabla ya kutumia mfumo.

  • Kusimamia usimikwaji wa Mtandao Kiambo (LAN), Mtandao Mpana (WAN) na Mawasiliano ya Ndani ya simu za mezani (PBX) katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Halmashauri ya Jiji la Arusha, Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mt. Meru chini ya Mradi wa GovNet.
  • Kusimamia usimikwaji wa Mfumo wa mahudhurio "Biometric Time and Attendance Monitoring System” umesaidia kuongeza ufanisi wa kazi kama watumishi kuwahi kazini, kuacha utoro pia mfumo umesaidia kuboresha utoaji wa huduma, nidhamu kwa watumishi.
  • Kusimamia maboresho ya Website ya Mkoa (www.arusha.go.tz) na matumizi wa email za serikari (GMS- Government Mailing system)
  • KITENGO CHA UHASIBU 
  •  
  • Kutoka na kitengo kutekeleza vizuri kazi zake tumeweza kuiletea hati safi ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
  • Kutokana na utunzaji mzuri wa kumbukumbu za madeni kwa mwaka ulioishia 2016/2017 Mkoa umeweza kupatiwa fedha za madeni kiasi cha shilingi 2,033,496,410.00 na kuweza kulipa madeni ya watumishi,wazabuni na wakandarasi.
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kupitia kitengo chake cha uhasibu imekuwa ikiwajali watumishi wake na kuhakikisha wanapata stahili zao kwa wakati pindi fedha zinapokuwepo bila usumbufu.ikiwa Extra duty kwa watumishi wa kada za chini,utilities kwa viongozi,fedha za likizo, Stahili za Madaktari na wauguzi  na stahili nyinginezo.
  • Kwa kutumia mtandao wa malipo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imeweza kuwezesha ulipaji wa malipo wa moja kwa moja kwenye Akaunti za watumishi na wazabuni kwa njia ya TISS na kuondoa usumbufu wa kwenda na hundi Benki.
  • Kwa kutumia Mtandao wa malipo utengenezaji wa Hesabu za Mwaka umerahisishwa na hesabu zinapatikana kwa wakati na bila usumbufu.
  • 12.0 HITIMISHO

Tangu Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Novemba 2015 imeendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015 – 2020, kama Mkoa mambo mengi yatatekelezwa katika kuinua uchumi, ujenzi wa miundombinu, uboreshaji wa huduma za Afya, Elimu, Ukusanyaji wa mapato na utumiaji sahihi wa mapato ya Serikali.

Lengo ni kumsaidia mwananchi mnyonge na kuboresha maisha ya jumla ya wananchi kwa kutumia rasilimali zilizopo.

Jukumu la wananchi ni kuunga mkono juhudi za Serikali chini ya Uongozi wa Rais John Pombe Magufuli na wasaidizi wake wote.

MRISHO MASHAKA GAMBO

MKUU WA MKOA

ARUSHA

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa