KATIBU TAWALA MKOA WA ARUSHA AFANYA ZIARA MERU ASISITIZA UMALIZIAJI WA MIRADI KWA WAKATI .
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Musa amefanya ziara katika halmashauri ya Wilaya ya Meru,Wilayani Arumeru ambapo amepongeza ujenzi wa miradi ya kituo cha afya Mareu na Maroroni na kuhimiza miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi .
Akizungunza wakati alipotembelea mradi wa Kituo cha afya Mareu, ambacho Serikali ya awamu ya Sita ikiongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ilitoa Milioni 500 fedha za tozo ya Miamala ya simu kwaajili ya ujenzi wa Jengo pacha la mama na mtoto na upasuaji, jengo maabara, nyumba ya watumishi wa tatu
Wananchi takribani 121,912 wanatarajia kunufaika na huduma za Afya zitakazotolewa na kituo cha Afya Mareu katika kata ya King'ori malula, Kikatiti na Leguriki Wilayani Arumeru.
Majengo mbalimbali yamejengwa ikiwemo jengo la Mama na Mtoto, chumba cha upasuaji, jengo la mionzi, Maabara, vyumba ya watumishi na jengo la kufuria.
Bwana Missaile Musa amesema hatua iliyofikiwa ya ujenzi ni nzuri na Halmashauri ihakikishe majengo yanakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Amesema wananchi wa kata 3 wanatarajia kupata huduma za Afya katika kituo hicho hivyo wajitaidi kumaliza ujenzi uliobaki.
Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) imenunua vifaa kwa ajili ya kituo hicho.
Kutokana na kukamilika kwake mapema itarahisisha huduma kuanza kutolewa kwa wakati.
Katibu Tawala amefanya ziara ya kikazi katika halmashauri ya Meru na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo vituo vya Afya na ofisi za tarafa.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa