Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Arusha Mhandisi Justine Rujomba amemueleza mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kuwa wizi wa maji na mita za maji ni changamoto kubwa inayodumaza upatikanaji wa maji safi na salama kwenye jiji la Arusha.
Kwenye kikao kazi kilichoitishwa na Mhe. Makonda ili kujadili hali ya upatikanaji wa maji mkoani Arusha, Mhandisi Rujomba amemuambia Mkuu wa Mkoa kuwa wizi huo wa maji unafanywa zaidi na watu wenye pesa na sio maskini kama inavyodhaniwa na wengi.
"Wanaoiba maji Mheshimiwa Mkuu wa mkoa ni wale wenye pesa, tunawakamata wanaiba maji kwahiyo maji yameingia lakini na kasumba ya watu wenye hela hawapendi kulipa maji kutokana na taratibu za serikali zilizowekwa" amesema Rujomba.
Katika hatua nyingine Mhandisi Rujomba pia ameitaja changamoto nyingine ya upotevu wa maji kwenye Jiji la Arusha, akisema hali hiyo inasababishwa na uchakavu wa miundombinu mingi inayotumika kusambaza na kusafirisha maji kwenye jiji la Arusha.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa