• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

MFUMO WA iMES UTAONGEZA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI KATIKA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA SERIKALI....

Posted on: November 8th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Imeelezwa kuwa, ikiwa mpango wa Serikali wa kutumia Mfumo Jumuishi wa Kutathmini Utekelezaji wa shughuli za Serikali ( iMES), ukisimamiwa vizuri, utawezesha watumishi kufikia malengo ya Serikali, ya kutoa huduma bora kwa wananchi, kwa kuwa mfumo huo unauwezo wa kuonesha hatua za utekelezaji wa shughuli zote za Serikali hatua kwa hatua.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K. Mongella, wakati akifunga mafunzo ya mfumo huo kwa Wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo, mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa mkoa kwa usimamizi wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI.


Mhe. Mongella amesema kuwa mfumo huo, ukitumika kwa welezi,  utampa kila msimamizi wa mradi kutekeleza majukumu yake bila kusukumwa na kusaidia miradi kutekelezeka kwa wakati na kukamilika kwa ufanisi na kwa mafanikio makubwa.


Hata hivyo, Mhe. Mongella, amewataka wakurugenzi wa halmashauri, kuwajengea uwezo watendaji wa chini wanaohusika katika usimamizi wa miradi, wakiwemo Walimu na Maafisa Watendaji wa kata na vijiji, ili kuwa na uelewa wa pamoja wa kuhakikisha mfumo wa iMES unafanyakazi kwa weledi na kufikia malengo ya serikali.


Aidha, ameipongeza Ofisi ya Rais TEMISEMI kwa kuja na mfumo rahisi wenye gharama nafuu, ambao utaondoa tabia ya kufanya kazi kwa mazoea, huku ukimsukuma kila mtumishi kuwajibika kwa nafasi yake kwa kuwa mfumo huo, unaruhusu kupima na kutathmini hatua zote za utekelezaji wa mradi.


"Mfumo huu unawapa nafasi Wakurugenzi kusimamia shughuli zote kupitia mfumo na kufahamu hatua zote za utekelezaji wa mradi kama unachelewa kuweza kuchukua hatua na kutambua ukwamishaji umefanywa na idara gani, mfumo umerahisisha kazi lakini unambana kila mtumishi kusimamia na kutekeleza majuku yake bila kusukumwa"


Naye Mkurugenzi wa TEHAMA Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Erick Kitale, ameeleza kuwa dirisha hilo la taarifa 'dashboard' linauwezo wakuchukua majira nukta 'code nates' za eneo husika, hali ambayo itakuwezesha kuona hatua za mradi bila udanganyifu badala ya kutumiwa picha za mradi mwingine jambo ambalo lilisambabisha udanganyifu katika hatua za utekelezaji wa miradi ya amendeleo.


Mfumo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini (Intergrated Monitoring and Evaluation System)  iMES, umeandaliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.


Awali Mkurugenzi Msaidizi, Divisheni ya Sera na Mipango, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Mwacha, ameyataja malengo ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wakurugenzi na maafisa TEHAMA, ili waweza kutumia mfumo huo Jumuishi wa ufuatiliaji wa shughuli zote za serikali kisekta.


Ameeleza kuwa awali kulikuwa na changamoto katika ufuatiliaji wa utekeelezaji wa shughuli za maendeleo hususani katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kulingana na thamani ya fedha, matumzii ya fedha pamoja na muda wa utekelezaji wa mradi husika.


"Faida za mfumo huu tofauti na mifumo iliyotangulia, mfumo unaonesha mahali mradi ulipo kwa kuzingatia code nates zake,  idadi ya miradi na gharama zake, matumizi ya fedha, maendeleo ya mradi na hatua zilizoendelea na zilizofikia, miradi ya bakaa na fedha zake" Ameweka wazi Mwacha


Mafunzo ya hayo ya Mfumo jumuishi yametoleaa kwa Wakurugenzi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri saba za mkoa wa Arusha.



Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa