• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

MHE. RAIS, DKT. SAMIA ACHANGIA MILIONI 100 UJENZI WA KANISA KATOLIKI PAROKIA YA KAROLI LWANGA...

Posted on: April 29th, 2024

Na Elinipa Lupembe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi milioni 100 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa jengo jipya  la Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha Parokia ya Karoli Lwanga  eneo la Usa- River, wilaya ya Arumeru

Akizungumza wakati wa kukabidhi sadaka hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, ambaye amemuwakilisha Mheshimiwa Rais kwenye Harambee hiyo, amesema kuwa, Mhe. Rais amemuagiza kuwasilisha sadaka yake, yeye na familia yake ya shilingi milioni 100.

Mhe. Makonda ameweka wazi kuwa, licha ya sadaka hiyo, Dkt. Samia amemuagiza kufikisha salamu zake za upendo, zinazokwenda kufanikisha ujenzi wa nyumba ya Bwana, Sadaka ambayo ameiombea ikadumishe Umoja na Mshikamano ndani ya Kanisa na Taifa kwa ujumla wake.

"Ninaamini waumini hawa wameweka nia moja ya kumjengea Mungu Kanisa, naungana na waumini wa Parokia ya Karoli Lwanga, kutimiza dhamira yao katika kumtumikia Mwenyenzi Mungu, sadaka hii ikasimame katika upatanishi na kujenga umoja wa Kanisa na Taifa letu la Tanzania" Mhe. Makonda amenukuu salam za Dkt. Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan

Hata hivyo, Mhe Makanda ametoa Mchango wa  shilingi Milioni 10, na  kuiombea sadaka yake, ikanene mema na kuwa baraka kwa wakazi wote wa Arusha kwa kuondoa mapooza pamoja na kuitakasa ardhi Arusha dhidi ya ajali zote zinazoondoa uhai wa watu wengi hasa watoto wadogo wenye ndoto za kutimiza.


Aidha, ametumia nafasi hiyo kuuombea uzao wa wanaarusha kuwa wenye baraka huku akihimiza wakazi wote na kumtanguliza Mungu na kuwa na hofu ya Mungu katika maisha yao ya kila siku,  ili kuendelea kuneemeka na baraka zake.


Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga ilianzishwa mwaka 1975 na kujengwa kanisa lililokuwa na uwezo wa kubeba waumini 600 kwa wakati mmoja na kulingana na wingi wa waumini kwasasa, Kanisa hilo limeamua kujenga kanisa jipya litakalokuwa na uwezo wa kubeba waumini 2500 kwa wakati mmoja.


Awali, Jengo jipya linakadiriwa kutumia shilingi Bilioni 2.7 ulianza mwaka 2010 umefikia 54% ukigharimu bilioni 1.4 na kusalia Bilioni 1.3.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa