Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella amevitaka vikundi vya wakulima na wafugaji Mkoa wa Arusha (MVIWAARUSHA) kubadili vikundi hivyo viwe vya nguvu ya kiuchumi.
Ushauri huo ameutoa alipokuwa akifungua mkutano Mkuu wa 9 wa mtandao wa vikundi vya wakulima na wafugaji wa Mkoa wa Arusha,katika chuo cha misitu.
Amesema vikundi hivyo vikiwa na nguvu ya kiuchumi itasaidia hata uchumi wa mtu mmoja mmoja kuimarika, kisha wakifamilia na nchi kwa ujumla.
Wakiwa wanasherekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania bara na miaka 20 ya umoja huo wajitaidia kubadili mitazamo ya namna ya uwendeshaji wa vikundi hivyo ili viweze kuleta tija.
Amewashauri wakulima kubadili namna ya uuzaji mazao yao kwa kuyachakata kwanza na kuyaweka katika vifungashio vizuri vyenye lebo na kukuza nje ya nchi badala ya kuyauza yanapotoka shambani tu.
Vile vile wafugaji wameshauriwa kufuga kisasa hasa kwa kuanzishi Viwanda vidogovidogo kupitia vikundi vyao vitakavyoweza kuchakata mazao yatokanayo na mifugo na kuyauza.
Mongella amesisitiza kundi la wakulima na wafugaji ni kundi linalotegemewa sana katika kuleta mchango mkubwa wa maendeleo hivyo wanatakiwa kubadilika na kufanya kazi zao kisasa zaidi.
Mwenyekiti wa MVIWAARUSHA bwana John Mayo amesema mtandao huo wa wakulima na wafugaji unavikundi takribani 457 vyenye wanachama 11,089 kutoka katika Halmashauri ya Karatu, Arusha, Meru, Monduli, Longido na Ngorongoro.
Amesema mtandao huo umewasaidia wakulima wengi kufanya kazi kwa amani na mashikamano.
Nae, Mratibu wa MVIWAARUSHA bwana Richard Masandika amesema mtandao huo umejikita zaidi katika kuwainua wakulima wadogo ambao wanamchango mkubwa katika kuzalisha chakula katika nchi kwa asilimia 75.
Mpaka sasa watu zaidi ya asilimia 60 hadi 65 wamejikita katika shughuli za Kilimo na ufugaji kwa nchi nzima.
MVIWAARUSHA, wamekutana katika mkutano wao wa mwaka kwa lengo la kujengeana uwezo kupitia changamoto walizonazo na pia kuchagua uongozi mpya wa mtandao huo.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa