• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

MIFUMO MIPYA YA UTENDAJI KAZI SERIKALI INAENDA KUWABANA WATUMISHI WASIOFANYA KAZI..

Posted on: December 16th, 2023

Na Elifuraha Laizer


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (MB), amesema, matumizi ya mfumo wa PIPIMS, PEPMIS na HR Assesment  katika Utumishi wa Umma nchini, inakuja kufanya tathmini kwa watumishi wa Umma pamoja na kuwabana Watumishi wasiotekeleza majukumu yao na kufikia malengo yaliyowekwa.


Mhe.Kikwete amesema hayo, wakati akizungumza  na Watumishi wa  Ofisi ya  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, kwenye kikao kifupi kilichofanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha , 15 Desemba 2023.


Ameeleza kuwa, Serikali imedhamiria kuimarisha Utumishi wa Umma kwa kuhimiza uwajibikaji na kuhakikisha, Taifa linakuwa na utumishi wa Umma unaopimika kwa kumpima Mtumishi mmoja mmoja pamoja  na Taasisi kwa ujumla.


"Mfumo wa PEPMIS umekuja kuwa mbadala wa OPRAS, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amelenga kuimarisha mifumo ya uwajibikaji, inayowezesha viongozi na watumishi wa Umma kuendelea kutekeleza majukumu yao, kwa ufanisi wakati na mahali popote, na zaidi kuwabana watumishi wanaopenda kukaa ofisini pasipo kufanya kazi" Amebainisha Naibu Waziri huyo


Aidha, Mhe. Kikwete amewataka Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala, kuacha kukaa ofisini badala yake,  watembelee maeneo yote ya kazi, na kusikiliza changamoto zinaziwakabili watumishi walio chini yao na kuweza kuzitatua kwa wakati.


Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.John V.K Mongela, amemshukuru Naibu Waziri huyo kwa kufuatilia utoaji wa mafunzo unaoendelea katika mkoa huo, na kusisitiza kuwa, kutokana na kukua kwa teknolojia, zama hizi hazihitaji watu wenye misuli badala yake wenye kuwajibika katika kazi.


Ameongeza kuwa, mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka,  ambapo Maafisa Tawala, Utumishi na Rasilimali Watu, watabadilika kuendana na teknolojia na kuachana na utaratibu wao wa utendaji kazi wa kizamani.


Hata hivyo ametumia fursa hiyo kuiomba Ofisi ya Rais,  UTUMISHI na Utawala Bora kuwanoa upya Maafisa Tawala, Utumishi na Rasilimali Watu,  wa mikoa na Halmashauri kwani utendaji wapo ambao utendaji kazi wao, sio wa kuridhisha, kwa kuzingatia, wao ndo wenye jukumu la kuwasimamia watumishi wengine.

#ArushaFursaLukuki

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa