• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

MILIONI 981.3 ZATOLEWA KWA WALENGWA WA TASAF MKOA WA ARUSHA: WAMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA

Posted on: November 8th, 2024


Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa  na Mhe.  Rais Dkt. Samia Suluhu hassan, imeendelea kutekeleza mpango wa kunusuru kaya masikini mradi unaoteklezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 981.3 kwa  walengwa walio kwenye mpngo huo, Mkoa wa Arusha.


Akizungumzia na mwandishi wa habari hizi, Mratibu wa TASAF Mkoa wa Arusha, Richard Nkini amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kimetolewa kwa kaya 41,272 ikiwa ni ruzuku ya mwezi Julai na Agosti 2024 kwa halmashauri zote saba za mkoa wa Arusha.


Amefafanua  kuwa, fedha hizo ni mahsusi kwaajili ya ruzuku ya Msingi, Elimu pamoja na afya ili kuhakikisha walengwa hao wanapata mahitaji yao ya msingi ikiwa ni pamoja na  watoto wa kaya hizo kupata mahitaji muhimu ya kuwawezesha kuhudhuria masomo na kliniki kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.


Fedha hizi licha ya kuwasaidia walengwa kuapata mahitaji ya familia lakini zaidi zinawawezesha kuanzisha miradi midogo midogo ya kuinua pato la familia na hatimaye kutoka kwenye lindi la umasikini uliokithiri". Amesema Nkini.


Hata hivyo wanufaika hao wameishukuru Serikali yao ya awamu ya tano, kwa kuendelea kuwajali wananchi wa kipato cha chini, kwa kuwa kabla ya kuwepo kwa mradi huo wengi walishindwa kuendesha maisha yao na familia zao, kutokana na hali ngumu maisha iliyosababishwa na kipato duni.


Mmoja wa wanufaika hao, Bibi Zuhura Ally ambaye ni mkazi wa Kata ya Ngarenaro amesema kupitia fedha hizo, anamudu kuwasomesha wajukuu wake ambao ni yatima kwa kuwnunulia mahitaji ya shule matumizi huku akutumia fedha nyingine kwa matumizi ya familia, jambo ambalo hapo awali ilikuwa ni ngumu kwake na familia.


Ninaishukuru Serikali kwa kutujali, mimi ninalea wajukuu zangu ambao ni yatima, ninamshukuri Mungu, huu mradi wa TASAF umetusaidia wengi, kabla ya hapo tulikuwa na hali ngumu ya maisha". Amesema Bibi Zuhura.


Ikumbukwe kuwa, mradi wa Kunusuru kaya Masikini nchini ni utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA WAKUU WA MAJESHI YA ULINZI (SADC).

    May 30, 2025
  • SAMIA MOTOCROSS CHAMPIONSHIP KUREJEA MSIMU WA PILI JULAI 12, 2025

    May 27, 2025
  • MKOA WA ARUSHA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUBWA WA WAKUU WA MAJESHI WA SADC

    May 25, 2025
  • UJENZI WA UWANJA WA AFCON ARUSHA SIO MICHEZO TU, NI FURSA YA KIUCHUMI

    May 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa