*Amshukuru Dr Samia kutoa Bilioni 32.5 za kutekeleza miradi hiyo*.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Makalla amewaagiza wakandarasi wanaotekeleza miradi ya kimkakati Jiji la Arusha ikiwemo ujenzi wa Kituo kikuu cha mabasi Mkoa, Soko la Kilombero na Jengo la Utawala Jiji la Arusha, kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati, ifikapo Mei 2026, kulingana na mikataba ya ukamilishaji wa miradi hiyo.
CPA Makalla ametoa wito huo leo Oktoba 13, 2025 wakati alipotembelea na kukagua hali ya utekelizaji wa miradi ya maendeleo Jiji la Arusha, miradi inayotekelezwa kwa gharama ya shilingi 32.5 fedha zilizotolewa na serikali kwa lengo la kuboresha miundombinu ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi wa mkoa wa Arusha.
"Niwatake wakandarasi kama mikataba yenu inavyojieleza kwenye mradi ya Stendi na Soko kukamilika Mei 2026, ikamilike na kwa viwango vya ubora unaoendana na thamani ya fedha, ili ifikapo Juni 2026, miradi hiyo ianze kufanya ya kuwahudumia wananchi.
Aidha, amemshukuru Rais wa Serikali ya awamu ya sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 23.5 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo mikubwa ya kimkakati, miradi ambayo inakwenda kujenga na kuboresha mandhari ya jiji la Arusha kwa kuboresha huduma za usafiri na mazingira ya ufanyaji wa biashara ndani ya Mkoa wa Arusha.
"Nitumie fursa hii kumshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi mikubwa yenye mabilioni ya fedha, miradi inayoonesha dhamira ya dhati ya Dkt. Samia ya kuhakikisha wananchi wanapata huema bora na kwa wakati kwenye majengo mazuri na ya kisasa". Amebainisha CPA Makalla.
Hata hivyo miradi hiyo ya ujenzi wa Kituo kikuu cha mabasi ya Mkoa wa Arusha utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 14, ujenzi wa Soko la Kilombero utakaogharimu shilingi Bilioni 9.5 na Jengo la utawala shilingi Bilioni 9, miradi ambayo iko hatua za awali na inayegemea kukamilika mapema Mei, 2026.
Awali, wananchi wa maeneo ambayo inatekelezwa miradi hiyo, wameishukuru Serikali kwa kuanza utekelezaji wa miradi hiyo ya kimkakati, miradi inayokwenda kutatua changamoto ya Kituo cha
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa