• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

MKOA WA ARUSHA WAINGIZWA KWENYE PROGRAMU YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA YA LIPA KUTOKANA NA MATOKEO (PforR)

Posted on: October 11th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Hatimaye Mkoa wa Arusha umekuwa ni miongoni mwa mikoa nane nchini, kwa kufanikiwa kuingizwa kwenye program endelevu ya maji na usafi wa mazingira vijijini, program ya Lipa kutokana na Matokeo (P4R).


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo kwenye kikao kazi kilichowakutanisha viongozi na watalamu wa sekta mtambuka kutoka wilaya tano za mkao wa Arusha,  Mkuu wa mkoa huo Mhe. John Mongela ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia kwa kuona umuhimu wa kuuingiza mkoa wa Arusha kwenye programu hiyo muhimu kwa wananchi wa mkoa huo, mradi wenye lengo la kuongeza upatikanaji wa maji vijijini ifikapo 2025.


Amebainisha kuwa mkoa wa Arusha unakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji, kutoaka na wananchi wa mkoa huo ni wakulima na wafugaji wanaotegemea maji kwa kiasi kikubwa huku asilimia 70 ya maeneo ya mkoa huo yanakabiliwa na  ukame kwa kipindi kirefu cha mwaka, hivyo kukamilika kwa mradi huo unakwenda kutatua changamoto ya maji kwa wananchi waishio vijijini.


"Kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Arusha, tunamshukuru mheshimiwa Rais kwa jitihada kubwa za kutatua changamoto za wananchi waishio vijijini kwa kusogeza huduma muhimu ikiweomo maji, hivyo niwatake viongozi wa wananchi, wa siasa, wa dini kushirikiana na watalamu kiwaelimisha wananchi kutambua umuhimu wa mradi huu endelevu" Amesema Mhe. Mongella.


Fedha za program hii ni Lipa kutokana na Matokeo (PforR) mkoa umepewa kama mbegu, ambayo programu hii ikatekelezwa vizuri serikali italeta fedha nyingi zaidi za kutekeleza miradi ya maji na hatimaye uhaba wa maji  mkoa wa Arusha kuwa historia, hivyo ni vema kila mtu kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huu.


Mwenyekiti wa Bodi ya TARURA Tanzania Mhandisi Ruth Koya amewasisitiza watalamu kushirikiana na viongozi wa wananchi kuelezea vizuri manufaa ya mradi huu na kuongeza kuwa anaamini kukamilika kwa program hiyo kutasaidia kufikia adhma ya serikali ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kuhakikisha maji yanapatikana karibu na makazi ya watu.


Naye Meneja wa TARURA mkoa wa Arusha Mhandisi Joseph Makaidi, amesema kuwa, programu hiyo itagharimu shilingi bilioni 4.8 na kutekeleza miradi 28 ya maji kwenye wilaya tano za mkoa wa Arusha, wilaya ya Arumeru, Monduli, Longodo Karatu na Ngorongoro, huku kila wilaya ikapata shilingi milioni 961.


Amesema kuwa, kukamilika kwa miradi hiyo kutaongeza asilimia 6 ya upatikanaji vijijini, huku miradi 24 inayoendelea kuongeza asilimia 6 na kufikia asilimia 85 za upatikanaji wa maji safi na salama vijijini ifikapo mwaka 2025 katika mkoa wa Arusha.


"Programu hii ina malengo ya kuwezesha upatikanaji wa maji vijijini, kuboresha huduma za usafi wa mazingira na usafi binafsi unatekelezwa na wizara ya maji na kusimamiwa na  RUWASA, wizara ya Afya na wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia"Amefafanua Mhandisi Makaidi


Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Daudi Kolimba, licha ya kuishukuru serikali kwa programu hiyo inayokwemda kutatua changamoto ya ukosefu wa maji safi ja salama vijijini ameahidi kwenda kusimamia hatua zote za utekelzaji wa miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na viwanho vya ubora vilivyokubalika na kifikia lengo la serikali la kuwahudumia wananchi


Ikumbukwe kuwa utekelezaji wa mradi wa maji unakwenda sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapindui ya mwaka ya kuhakikisha  kufikia asilimia  85 ya uaptikanaji wa maji safi na salama vijiji na asilimia 95 mijini ifikapo mwaka 2025.


#KaziInaendelea







Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa