OR-TAMISEMI
Naibu Waziri anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali imekuja na Mpango wa Shule Salama kwa shule za Msingi na Sekondari ambao ni shirikishi na jamaii ili kudhibiti mdondoko wa wanafunzi.
Mhe. Katimba ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo kwa Wenyeviti wa Bodi za Shule za Sekondari, Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Kata pamoja Maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii ngazi ya Mkoa kuhusu Mpango wa Shule Salama na Usimamizi wa Usalama wa Jamii katika chuo cha Patandi mkoani Arusha leo tarehe 18.08.2024.
Amesema Serikali imekwishafanya jitihada za kudhibiti mdondoko wa wanafunzi ikiwa ni pamoja kutoa Elimu bila Ada ili kupunguza vikwazo katika uandikishaji wa wanafunzi, kujenga shule za Msingi na Sekondari karibu na makazi ya wananchi ili kupunguza adha kwa wanafunzi kutembea umbali mrefu, Kuimarisha mifumo ya utambuzi wa wanafunzi ambao wapo kwenye hatari ya kuacha shule, Kuimarisha utaoaji wa huduma na ushauri na unasihi pamoja na Kuandaa Mwongozo wa kuwarejesha Shule Wanafunzi walioacha Shule.
Mhe. Katimba ameongeza kuwa pamoja na jitihada hizo changamoto ya mdondoko wa wanafunzi katika Shule za Msingi na Sekondari haijakwisha kabisa na Kasi ya kupungua kwa idadi ya wanafunzi wanaocha shule haijakwisha kabisa.
“Uchambuzi wa sababu za kutokwisha kwa mdondoko wa wanafunzi unaonesha kuwa mazingira yasiyo salama kwa wanafunzi wakiwa shuleni na wakati wa kwenda na kurudi shuleni yanachangia kwa kiasi kikubwa kutokushuka kwa kiwango cha mdondoko wa wanafunzi”.
Ili kuweka mazingira ya shule yaliyosalama Serikali iliona ni vyema kuja na mkakati mpya unaojulikana kama Mpango wa Shule Salama katika Shule za Msingi na Sekondari nchini.
Serikali imedhamiria kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa Kuimarisha ushiriki wa wazazi/walezi na Jamii katika kusimamia ufundishaji na ujifunzaji pamoja na mahudhurio ya wanafunzi’.
Kuimarisha mifumo ya kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanafunzi katika Elimu ya Msingi na Sekondari na
Kuimarisha utoaji wa huduma ya Chakula na Lishe kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa