Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, Godfrey Eliakimu Mnzava amezindua mradi wa ujenzi wa vyumba 15 madarasa, mabweni 2 na matundu 21 ya vyoo 21 Shule ya Sekondari ya Wasichana Arusha kata ya Olasiti, mradi uliotekelezwa na serikali kupitia Kampuni ya madini Barrick kwa gharama ya shilingi milioni 679.1
Amesema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira rafiki ya wadau kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, miradi inayokwenda kusogeza huduma kwa wananchi.
Tunaishukuru Kampuni ya Barrick kwa mchango wake mkubwa kwa jamii, serikali inatambu na kuthamini kazi hii kubwa na ya kizalendo iliyofanywa, inayowezesha watoto wa kitanzania kupata elimu kwenye mazingira rafiki
Aidha amewataka walimu kuwasimamia wanafunzi kutunza miundombinu hiyo iliiweze kudumu kwa muda mrefu na kuwanufaisha watoto kwa sasa na vizazi vijavyo.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 ni "Tunza Mazingira, Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu"
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa