Halmashauri za wilaya ya Monduli,longido na Arumeru zimetakiwa kufanya jitihada zaidi katika uchangiaji wa fedha zinazotengwa na halmashauri kwa ajili ya lishe ili kupunguza changamoto ya lishe duni kwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Ni katika kikao cha kujadili mwenendo wa hali ya lishe ndani ya mkoa wa Arusha ambapo Pamoja na mambo mengine suala kubwa linalojadiliwa ni kuhakikisha halimashauri zote zinachangia fedha kwa ajili ya lishe ambapo msisitizo unawekwa kwa zile halimashauri ambazo hajifikia lengo kufanya hivyo mara moja.
Mosses Mabula-Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya lishe ya mkoa amesema
Mikakati ya kubadilisha hali ya lishe katika mkoa wa Arusha inawekwa ikiwa ni Pamoja ni kuhamasisha halmashauri ambazo hazijatekeleza mpango huo wa kuchangia na kutumia fedha za lishe kufanya hivyo ili mkoa huo kurudi katika alama ya kijani.
Rose Mauya-Afisa Lishe mkoa wa Arusha naye alisisitiza Ushirikishwaji wa wananchi katika mpango huo wa lishe ni jambo linalopewa kipaombele ili kutoa elimu ya uelewa katika suala hilo
Haya yanajiri ikiwa ni jitihada za kufanya mkoa wa Arusha kuwa na alama nzuri katika suala la lishe bora.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa