• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

OFISI YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA WASHERHEKEA MWAKA MPYA NA WATOTO WAISHIO KWENYE MAKAO...

Posted on: January 2nd, 2024


Na Elinipa Lupembe

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, chini ya uongozi wa Mhe. John V.K Mongella, wameshehekea Sikukuu ya mwaka mpya na watoto wanaolelewa kwenye Makao ya watoto wanaotoka kwenye mazingira magumu kwa kushiriki pamoja chakula cha mchana.

Akizungumza wakati wa kuwakaribisha wageni kwenye hafla hiyo, Mhe. Mongella, amesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida wa ofisi yake, ukiwa na lengo la kukaa na kula pamoja na watoto hao kama familia kwa kuthamini uwepo wa watoto hao pamoja na kazi kubwa inayofanywa na walezi wa watoto hao kwa niaba ya Serikali.

Serikali inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na walezi wa watoto katika Makao, kama watanzania na kwa niaba ya Serikali tunaungana nao kwa kidogo kinachopatikana ikiwemo kukaa pamoja na kushiriki chakula angalau mara chache panapo nafasi.

"Niwatie moyo watoto na vijana, mjisikie mko nyumbani na tushiriki pamoja chakula huku mkitambua changamoto mnazopitia ni sehemu ya maisha ambayo humkuta binadamu yoyote, mshukuruni Mungu kwa nafasi ya malezi mliyopata na kutambua thamaninyenu kubwa kwa jamii" Ameweka wazi Mhe. Mongella

Hata hivyo wageni, viongozi pamoja na walezi wa watoto hao, wameishukuru Serikali kupitia Mkuu huyo wa mkoa,  kwa upendo mkubwa aliuonyesha kwa kuwathamini watoto hao wenye uhitaji na kusema kuwa huo ni moyo wa kipekee kwa kuwa kuwa kiongozi pekee haimaanishi unauwezo wa kutoa.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania, Askofu Dkt. Isarael Ole Gabriel Maasa, amesema kuwa, Mhe. Mongella ni kiongozi mwenye maadili anayemuheshimu Mungu, Sadaka aliyotoa ndio dini nzuri inayoelekezwa kwenye maandiko matakatifu.

"Mkuu wa mkoa, sadaka hii inakufanya uwe na dini safi, Maandiko yanasema, Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa"Amenukuu Kitabu cha Yakobo 1:27

Naye Shekhe Mkuu wa mkoa wa Arusha, Shaban Juma, amekiri kuwa, wapo watu kwenye Serikali lakini hawafikirii kuwaleta wanyonge kama hawa nyumbani kwao, Mtume anatuambia wapo watu wameumbwa kwa ajili ya haja za watu hasa wanyonge, Mkuu wetu wa mkoa ndio aina ya watu hao.

Dominic mtoto anayelelewa kwenye Makao ya The Joy of God Orphanage Center, amemshukuru Mkuu wa mkoa, kwa kuwakaribisha, kukaa meza moja na kula pamoja, kwa niaba ya watoto wenzake ametoa shukurani za dhati na kumuombea dua jema,  Mwenyenzi Mungu ambariki na abariki pale anapofanyia kazi

"Tunaishukuru Serikali haijawahi kutuacha, asante baba yetu kwa kutualika siku ya leo, tumekula, tumeshiba na tumefurahi sana, tunakuombea Mwenyenzi Mungu asikupungukie pale ulipotoa, lakini tunawaomba wengine wenye uwezo kuendelea kuwasaidia watoto wenye mahitaji ili wakue na wasome hatimaye waweze kufikia ndoto zao kama watoto wengine" Amesema Shazma Hassan wa Makao ya Dhi Nurney Ngaramtoni

Awali, hafla hiyo imejumuisha watoto 131 kutoka kwenye nyumba tano za Makao,  iliyofanyika nyumbani kwa mkuu huyo wa mkoa wa Arusha, eneo la Uzunguni, kata ya Sekei, Jiji la Arusha.




Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa