Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria katika kutimiza kikamilifu Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia kwa kuhakikisha kuwa inashughulikia na kutatua kwa haraka changamoto mbalimbali za kisheria zitakazowasilishwa kwenye Ofisi hiyo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza Johari ameeleza hayo leo Ijumaa Machi 28, 2025 Jijini Arusha kwenye viwanja vya Ngarenaro ikiwa ni uzinduzi wa siku kumi za utekelezaji wa kampeni hiyo kwenye Mkoa wa Arusha, Mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul Christian Makonda.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa tayari Ofisi yake imepokea malalamiko ya Wananchi waliopisha Ujenzi wa barabara ya Mianzini- Timbolo, akieleza kuwa Ofisi yake inaendelea kuwasiliana na Halmashauri husika katika kuhakikisha kuwa ufumbuzi wa changamoto hiyo unapatikana kwa wakati kwa Wananchi kupata stahiki wanazozidai Serikalini.
Hata hivyo, ametumia sehemu ya hotuba yake pia kualika Wananchi wa Arusha kujitokeza kwa wingi kuwasilisha malalamiko yao ya kisheria, akisema Ofisi yake ipo tayari kuwafikia, kuwasikiliza na kutatua kero za wananchi wa Mkoa wa Arusha kupitia Kampeni hiyo ya Msaada wa Kisheria iliyofadhiliwahiliwa na Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa