• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RAIS DKT. SAMIA ATOA BILIONI 42.34 KULIPA FIDIA KWA WANANCHI WA MKOA WA ARUSHA

Posted on: May 23rd, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa kiasi cha shilingi bilioni 42.34 kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha ili kumaliza migogoro ya ardhi na uendelezaji wa maeneo mbalimbali katika mkoa huo.



Akizungumza na wananchi wa Kata ya Moshono, Jijini Arusha, Mhe. Makonda amesema fidia hiyo imetolewa kwa maeneo kadhaa yaliyoguswa na miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa barabara, uwanja wa ndege, maeneo ya jeshi, na uchimbaji wa madini.



Katika Jiji la Arusha, eneo la Losirwa lililokuwa chini ya matumizi ya Jeshi limepewa fidia ya shilingi Bilioni 2.27, ambapo fidia hiyo imekwishalipwa, eneo la Oloresho kwaajili ya maandalizi ya mashindano ya AFCON, limetengewa fidia ya shilingi bilioni 7.27,  barabara ya Mianzini - Ngaramtoni nayo imelipwa fidia ya shilingi bilioni 3.49 ambapo fedha hizo zimelipwa tayari pamoja na eneo la barabara ya Mirongoine - Olmot limepokea fidia ya shilingi milioni 591.64 ambayo nayo imelipwa.



Aidha, Wilaya ya Arumeru, fidia kwa eneo la Jeshi lililopo Duluti imetolewa kwa kiasi cha shilingi bilioni 7.9 na tayari imelipwa yote kwa walengwa.



Wilaya ya Karatu imepata fidia ya shilingi bilioni 5.9 kwa ajili ya uwanja wa ndege wa Manyara uliopo katika eneo hilo, hatua inayolenga kufanikisha uboreshaji wa miundombinu ya usafiri wa anga.



Kwa upande wa Wilaya ya Monduli, eneo la Engaruka, ambalo linahusishwa na shughuli za uchimbaji wa madini ya magadi soda, limetengewa fidia ya shilingi bilioni 14.9, ikiwa ni sehemu ya uwekezaji wa kimkakati katika sekta ya madini.



Katika hatua nyingine, Mhe. Makonda amewataka viongozi wote wa Mkoa huo  kuacha mara moja tabia ya kuwaondoa wananchi kwenye maeneo yao bila kuwapa fidia stahiki, akisisitiza kuwa serikali ya awamu ya sita inalenga haki, usawa na maendeleo ya watu na ndiyo dhamira ya Rais Dkt. Samia katika kulinda haki za wananchi na kusukuma mbele ajenda ya maendeleo ya Taifa.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA WAKUU WA MAJESHI YA ULINZI (SADC).

    May 30, 2025
  • SAMIA MOTOCROSS CHAMPIONSHIP KUREJEA MSIMU WA PILI JULAI 12, 2025

    May 27, 2025
  • MKOA WA ARUSHA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUBWA WA WAKUU WA MAJESHI WA SADC

    May 25, 2025
  • UJENZI WA UWANJA WA AFCON ARUSHA SIO MICHEZO TU, NI FURSA YA KIUCHUMI

    May 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa